Watumiaji X (Twitter) sasa kufahamika walipo

November 27, 2025 5:01 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni kipengele ambacho kinaweka wazi taarifa muhimu kuhusu asili na mwenendo wa akaunti pamoja na mahali ambapo akaunti ilifunguliwa.

Dar es Salaam. Mtandao wa kijamii wa X (zamani Twitter) umeweka kipengele kipya kinachoweka wazi taarifa muhimu kuhusu ikiwepo mahali alipo mtumiaji wa akaunti hiyo, majina yaliyobadilishwa pamoja na mwaka ambao akaunti ilifunguliwa.

Maboresho hayo yanalenga kudhibiti matumizi ya akaunti feki pamoja na kusambaa kwa taarifa potofu, 

Kwa mujibu wa Mkuu wa Bidhaa wa X, Nikita Bier, hatua hiyo inalenga kuongeza uwazi na kuwapa watumiaji muktadha wa kutosha ili kutambua uhalisia wa akaunti.

Kipengele hicho kipya, kinaitwa About this Account, ambacho kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa kwenye mashirika ya habari ya The New York Times na BBC, kitaonyesha nchi ambako akaunti ilifunguliwa, mara ngapi mtumiaji amebadili jina la akaunti, pamoja na aina ya mfumo anaotumia kuendesha akaunti hiyo kama ni Android au iPhone.

Aidha, mtumiaji wa mtandao wa X anaweza kuangalia taarifa za “About this Account”  juu ya ukurasa wa wasifu wa mtumiaji anapoingia katika akaunti yake ya mtandao huo.

Mtumiaji atakapoingia katika ukurasa huo atatakiwa kubofya sehemu iliyoandikwa ‘Joined’ ambayo iko chini ya jina lake, aidha atakapofanya hivyo atapelekwa moja kwa moja kwenye ukurasa maalum unaoonyesha maelezo yanayohusu akaunti yake kwa kina.

Mtandao wa X ulianzishwa mwaka 2006 na Jack Dorsey, Evan Williams, Biz Stone na Noah Glass, kwa jina la awali ‘twttr’ kabla ya kubadilishwa kuwa Twitter. 

Twitter ilibadilishwa jina na kuwa X Julai 2023 mara baada ya kununuliwa na Bilionea Elon Musk mnamo Oktoba 27, 2022 kwa kiasi cha Dola 44 bilioni za Marekani sawa na Sh108 trilioni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow Us on TikTok

Subscribe to Our YouTube Channel

Subscribe

Loading videos...

Loading videos...

Loading videos...

Enable Notifications OK No thanks