Ahadi nne za CCM kukuza utalii Arusha

October 2, 2025 5:26 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Yalenga kuingiza watalii milioni 8 ndani ya miaka mitano ijayo.

Arusha. Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Samia Suluhu Hassan ameahidi kukamilisha miradi mikubwa minne itakayokuza utalii katika jiji la Arusha ikiwa atapewa nafasi ya kuongoza nchi kwa miaka mitano ijayo.

Samia aliyekuwa akinadi sera za chama hicho leo Oktoba 2, 2025  katika uwanja wa Amri Abeid jijini Arusha amesema lengo la kuendeleza miradi hiyo ni kufikia jumla ya watalii milioni 8 kwa mwaka.

“Lengo letu miaka inayokuja mpaka 2030 Tanzania ipokee watalii milioni 8 na hawa ni watalii wa ndani na nje ya nchi lakini pia lazima tuwekeze kwenye makazi na mahoteli…

….Tunakweda kuvutia wawekezaji wakubwa wajenge mahoteli ya nyota tano, nyota nne ili watalii waje kwa wingi wakiwa na uhakika wana sehemu nzuri ya kufikia,” amefafanua Samia.

Idadi hiyo ni mara nane zaidi ya wastani wa idadi ya watalii wanaoingia nchini Tanzania kwa mwaka Kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Maliasili na Utalii na Ofisi ya Takwimu (NBS).

Ili kufikia idadi hiyo Samia amesema wataongeza ndege nyingine tano ndani ya miaka mitano ijayo na kufanya jumla ya ndege nchini kufikia 21 kutoka 16 zilizopo.

Matukio mbalimbali katika picha kutoka uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha Mjini kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za uchaguzi mkuu CCM. Picha/CCM.

Pamoja na hayo, Samia amesema watakamilisha ujenzi wa kiwanja cha ndege Arusha kilichotumia Sh17 bilioni kitakachoanza kutumika Januari 2026  pamoja na na ujenzi wa kituo kipya cha mikutano.

“Tunakwenda kujenga kituo kipya cha mikutano ya kimataifa baada ya kile cha  AICC, tunajenga ukumbi mwingine mkubwa sana utakaokuwa na hoteli na fursa zote za mikutano ndani Jiji la Arusha…

…Kule Ngorongoro Lengani tunakwenda kujenga  kituo cha urithi wa kijeolojila kwa watalii watakaopenda mambo ya kihistoria, kisayansi na kijeolojia hicho kitakuwa kituo chao,” ameongeza Samia akifafanua miradi itakayofanywa akiingia tena madarakani.

Aidha, mgombea huyo amesema wataendeleza utalii wa kimichezo kwa kumalizia uwanja mpya utakaotumika katika mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) yatakayofanyika mwaka 2027.

Uwanja huo unatarajiwa kubeba watu 32,000, huku ukarabati wa miundombinu inayouzunguka ikiwemo barabara za ndani na nje ya mji  zinazotarajiwa kufungua fursa nyingi za kiuchumi kwa wakazi wa jijini hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow Us on TikTok

Subscribe to Our YouTube Channel

Subscribe

Loading videos...

Loading videos...

Loading videos...

Enable Notifications OK No thanks