Fahamu maeneo 3 yanayozalisha habari za uzushi mtandaoni
- Ni pamoja na majukwaa ya kigitali ya mtandaoni na vyombo vya habari visivyo rasmi.

Arusha. Mitandao ni miongoni mwa nyezo za upashanaji habari zinazotumiwa na watu wengi maeneo mbalimbali duniani ikiwemo nchini Tanzania.
Takwimu mpya za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) zilizotolewa hivi karibuni zinaonesha kuwa kufikia Juni, 2025 idadi ya watumiaji wa intaneti nchini imefikia milioni 54.1 ikiongezeka kutoka milioni 49.3 mwishoni mwa mwezi Machi, 2025.
Kuongezeka kwa watumiaji hawa hufanya majukwaa ya mtandaoni kuwa katika hatari ya kupokea taarifa za uzushi kutoka makundi mbalimbali ya watu yenye nia tofauti.
Miongoni mwa maeneo unayoweza kukutana na taarifa hizi za uzushi ni pamoja na mitandao ya kijamii, vyombo vya habari visivyo rasmi au blogu zisizosajiliwa na vyanzo visivyo halali vya kisiasa au watu binafsi wanaochochea propaganda.
Kumbuka kuthibitisha kila habari unayoiona mtandaoni ili uwe salama na wale wanaokuzunguka
Latest



