Kicheko: Bei ya petroli, dizeli ikishuka kwa mwezi Septemba Tanzania

September 3, 2025 9:57 am · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Bei ya petroli yafikia Sh2,807 na dizeli 2,754

Arusha. Kwa watumiaji wa mafuta ya petroli na dizeli huenda wakauanza mwezi Septemba kwa kicheko baada ya bei ya nishati hiyo kushuka kwa sh26 na Sh23 kwa lita mtawalia.

Ahueni hii inakuja ikiwa ni mwezi mmoja baada ya dizeli kupaa kiduchu kwa kwa Sh 10  hali iliyofanya watumiaji kutoboa mifuko yao kujipatia bidhaa hiyo.

Taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji Tanzania (Ewura) leo Septemba 3, 2025 inabainisha kuwa bei ya rejareja ya petroli  ni Sh 2,807 huku dizeli ikiuzwa kwa Sh2,754.

Bei hizo za reja reja kupitia bandari ya Dar es Salaam zimeshuka kutoka Sh2,843 kwa petroli na Sh2,777 kwa dizeli zilizokuwa zinatumika mwezi uliopita.

Kwa mujibu wa Ewura bei hio zimeshuka kutokana na kuongezeka kwa gharama za mafuta yaliyosafishwa (FOB) katika soko la Uarabuni.

“Katika bei kikomo kwa Septemba 2025, bei za mafuta katika soko la dunia zimepungua kwa asilimia 0.2 kwa mafuta ya petroli, asilimia 5.5 kwa mafuta ya dizeli na asilimia 3.5 kwa mafuta ya taa,” imesema taarifa ya Ewura.

Wakati bei hiyo ikishuka, gharama za kuagiza mafuta (premiums) katika Bandari ya Dar es salaam zimeongezeka kwa wastani wa asilimia 20.73 kwa mafuta ya petroli, asilimia 7.75 kwa mafuta ya dizeli na asilimia 2.62 kwa mafuta ya taa.

Pamoja na ahueni hiyo  bado wakazi wa Kyerwa (Ruberwa) ndiyo wanaonunua mafuta hayo kwa bei ya juu zaidi ya Sh3,079 kwa petroli na Sh3,027 kwa dizeli ikiwa ni Wastani wa Sh200 zaidi ya bei inayotumiwa na wakazi wa jiji la Dar es Salaam.

Follow Us on TikTok

Subscribe to Our YouTube Channel

Subscribe

Loading videos...

Loading videos...

Loading videos...

Enable Notifications OK No thanks