Maswali 5 ya kujiuliza kabla ya kuamini taarifa za uchaguzi mtandaoni

Arusha. Wakati Tanzania ikiajiandaa na uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu, ni kawaida kusikia au kuona taarifa nyingi zinazohusu tukio hilo katika mitandao mbalimbali ya kijamii.
Lakini kabla ya kusambaza au kuimini taarifa yoyote mtandaoni ni vyema kujiuliza maswali muhimu ambayo yanaweza kukusaidia kubaini ukweli katika taarifa hizo na kupunguza wimbi la kusambaza taarifa potofu au zilizoongezwa chumvi.
Miongoni mwa maswali hayo ni pamoja na kutathmini chanzo cha habari, Je, taarifa hiyo inatoka kwenye chanzo kinachoaminika kisheria? Mfano: Tume ya uchaguzi kama INEC, ofisi za serikali, au vyombo vya habari vilivyosajiliwa
Masuala mengine muhimu ya kuzingatia ni pamoja na kuangalia tarehe na muktadha wa taarifa, kutokuangalia kichwa cha habari pekee, kutafuta Uthibitisho kutoka kwa vyanzo vingine pamoja na kuchunguza piicha, video au vielelezo vya taarifa.
Latest



