Rais Samia amteua Prof Nagu Naibu Katibu Mkuu Tamisemi 

May 19, 2025 7:32 pm · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Prof Tumaini Nagu ameteuliwa miezi mitano baada ya kutenguliwa nafasi ya mganga mkuu wa Serikali
  • Pia amemteua Meja Jenerali Mstaafu John Julius Mbungo kuendelea kuiongoza Bodi ya Kampuni ya Meli Tanzania (Tashico).

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Prof Tumaini Nagu kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Tamisemi anayeshughulikia afya ikiwa ni miezi mitano baada ya kumtengua kiongozi huyo katika nafasi ya mganga mkuu wa Serikali.

Prof Nagu alienguliwa na Rais Samia kuwa Mganga Mkuu wa Serikali siku tatu baada ya Shirika la Afya Duniani (WHO) kuripoti uwepo wa ugonjwa wa Marburg Tanzania mkoani Kagera Januari mwaka huu uliogharimu maisha ya watu 10 kwa mujibu wa shirika hilo. 

Hata hivyo, leo Mei 19,2025 taarifa kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu imeeleza kuwa Prof Nagu ameteuliwa kushika wadhifa huo mpya ndani ya Tamisemi. 

Wengine walioteuliwa kwa mujibu wa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Moses Kusiluka amesema ni pamoja na Balozi George Kahema Madafa aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa bodi ya kampuni ya Puma Energy Tanzania, akichukua nafasi ya Dk Majige Budeba aliyemaliza muda wake wa uongozi.

Mshauri wa Rais masuala ya uchumi, Dk Blandina Kilama yeye ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango anayeshughulikia biashara na ubunifu. Dk Kilama ameteuliwa katika nafasi hiyo baada ya uteuzi wa Dk Lorah Madete kutenguliwa.

Rais Samia ameteua viongozi wengine kuongoza bodi mbalimbali za taasisi na mashirika ya umma. Walioteuliwa kuwe wenyeviti wa bodi kwa kipindi cha pili ni Jacob Jail Kibona wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) na Meja Jenerali Mstaafu John Julius Mbungo atakayeiongoza Bodi ya Kampuni ya Meli Tanzania (Tashico).

Wengine ni Mussa Hamza Mandia ameendelea kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) kwa kipindi cha pili mfululizo.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
7 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
7 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

Nukta TV