Dk Mpango aagiza udhibiti wa mifumo ya Serikali na uhalifu wa kimtandao

February 11, 2025 4:34 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link

Aitaka e-Ga kushirikiana na vyombo vingine vya usalama kufanikisha agizo hilo


Arusha. Makamu wa Rais wa Tanzania Dk Philip Mpango ameitaka mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) kuongeza nguvu ya katika ulinzi wa mifumo iya Serikali li kudhibiti uhalifu wa kimtandao.

Dk Mpango aliyekuwa akizungumza katika kikao kazi cha tano cha e-GA kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan leo Februari 11, 2024 jijini Arusha  amesisitiza mamlaka hiyo kushirikiana na vyombo vingine kudhibiti uhalifu huo.

“e-GA mnafanya kazi nzuri naomba muendelee kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)  na vyombo vingine vya dola kuhakikisha kwamba mnalinda usalama wa mifumo hii lakini pia kudhibiti uhalifu wa kimtandao,” amesema Dk Mapango.

Maagizo ya Dk Mpango yanakuja wakati Tanzania ikiendelea kupiga hatua katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) ikiwezesha baadhi ya huduma kutolewa kwa njia ya mtandao kupitia mifumo rasmi ya Serikali.

Miongoni mwa mifumo hiyo inayowezesha utoaji wa huduma kupitia mtandao ni pamoja na mfumo wa kusimamia rasilimali watu Serikali (e-watumishi), mfumo wa malipo serikalini (GPG) mfumo wa kusimamia hesabu za Serikali (MUSE), mfumo wa kuwezesha miamala ya malipo (Tips) na mfumo wa manunuzi ya Umma (Nest).

Benedict Ndomba, Mkurugenzi wa e-Ga amesema kuwa  mamlaka hiyo imeziwezesha taasisi za umma ikiwemo tovuti ya Serikali, tovuti ya ajira, na mfumo wa Bunge mtandao, yaani e-Parliament kutoa huduma kwa umma kupitia mifumo ya Tehama suala linalorahisha huduma kwa wananchi.

“Mifumo hii imeimarisha utendaji kazi wa taasisi husika, kusaidia kupunguza gharama kwa Serikali, kuboresha utoaji wa huduma kwa umma, na kulinda mazingira kwa kupunguza matumizi ya karatasi…”

…Ujenzi na uendeshaji wa mifumo na miundombinu hii unafanywa kwa kutumia wataalamu wazawa, jambo ambalo limewezesha serikali kuokoa fedha nyingi ambazo zingetumika kununua mifumo na kulipia leseni kutoka kwa wakandarasi wa nje ya nchi,” amesema Ndomba.

Kwa upande wake Joseph Kizito mhagama, Mwenyekiti wa Kmati ya kudumu ya Bunge, utawala na Sheria aliyekuwa akizungumza katika mkutano huo ameitaka Serikali kuhakikisha eGa inasimamia mifumo yote ya Serikali ili kulinda usalama wa taarifa za watumiaji pamoja na za Serikali.

Katika hatua nyingine Dk Mpango ameitaka eGa kuharakissha mchakato wa kuunganisha mifumo ya tasisi za umma na kuhakikisha inasomana  ili kurahisha upatikanaji wa taarrifa na utoaji wa huduma kama alivyoagiza Rais Samia.

“Niseme nimeridhishwa na hatua ya eGa kuanza utekekezaji wa agizo hili kwa kusanifu na kujenga mfumo huu wa ubadilishanaji taarifa Serikalini sasa ninawahimiza huo ukamilike kuhakikisha taasisi zote za umma zinajumuishwa katika mfumo,” amesema Dk Mpangi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Enable Notifications OK No thanks