Silinde awahimiza wakulima, wafugaji Mwanza kujiunga na vyama vya ushirika

October 21, 2024 6:09 pm · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Vyama hivyo vitawawezesha kupata mkopo wa kilimo kwa urahisi.

Mwanza. Naibu Waziri Wizara ya Kilimo, David Silinde amewahimiza wakulima na wafugaji mkoani Mwanza kuanzisha au kujiunga na vyama vya ushirika vya akiba na mikopo vilivyopo kwenye maeneo yao ili kuwaepusha kujiingiza katika mikopo umiza.

Silinde aliyekuwa akizungumza Jijini Mwanza leo Oktoba 21, 2024 ameeleza umuhimu wa wakulima hao kujiunga na vyama vya ushirika ikiwemo kujiwekea akiba na kuepuka mlolongo mrefu wa kupata mikopo kwenye taasisi nyiingine za kifedha.

“Nitoe rai kwa wananchi na wakulima kuona umuhimu wa kujiunga na ‘Saccos’ ili pindi wanapohitaji fedha kwa ajili shughuli za kilimo waweze kupata kwa urahisi kupitia kwenye Saccos zao,” amesema Silinde.

Aidha, Silinde amewataka viongozi na watendaji wa vyama hivyo vya Saccos kutoa elimu kwa wakulima ili waweze kupata uelewa wa kazi zinazofanyika ili kuwasaidia wakulima wengi kujiondoa kwenye vyama vinavyowaumiza.

Kwa upande wake Dk Benson Ndiege, msajili wa vyama vya ushirika nchini ametaja mafanikio yaliyofikiwa na vyama hivyo ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa amana za wachama kutoka Sh 897 bilioni hadi kufikia Sh 967 bilioni ukilinganisha taarifa ya mwaka 2022/23

“Lakini pia mikopo inayotolewa na vyama vya akiba na mikopo imeongezeka  na kufikia Sh1.11 trilioni kutoka Sh1.05 trilioni pia kuna ongezeko la wananchi kujiunga na vyama hivyo,” amesema  Dk Ndiege.

Baadhi ya wananchi na wanachama wa vyama vya ushirika vya akiba na mikopo wakiwa kwenye maadhimisho ya vyama vya ushirika yanayofanyika Jijiji Mwanza. Picha|Mariam John/Nukta.

Naye Hajjat Aziza Mshana,  Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Akiba na Mikopo Tanzania (Sccurt), amesema vyama hivyo vimeendelea kuimarika katika maeneo mbalimbali ikiwemo kuongezeka kwa mitaji, mali, wanachama na utoaji wa mikopo.

“Hivyo ni viashiria vinavyotupa nguvu ya kuendelea kuboresha zaidi  utendaji wa Saccos zetu,” amesema Hajjat Aziza.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Silinde ameagiza vyama hivyo vya Saccos kuacha kujiendesha kwa mazoea kwa kutumia makaratasi badala yake wawekeze kwenye mfumo wa Tehama katika kuboresha utendaji wao.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV