Bei ya ulezi yapaa Mtwara

September 5, 2024 5:01 pm · Davis Matambo
Share
Tweet
Copy Link

Bei ya gunia la kilo 100 la ulezi imepaa kufikia 400,000 kutoka 250,000 iliyorekodiwa Septemba 2, 2024 Mkoa wa Mtwara ikiongezeka kwa kiasi cha Sh150,000. Bei hii ni kubwa mara 6 ya bei ya chini iliyorekodiwa Ruvuma ambayo ni Sh60,000 tu.

Bei ya ngano Lindi imeendelea kusalia Sh400,000 ambayo ni mara sita zaidi ya ile inayotumika mkoani Rukwa ya Sh65,000 kwa gunia la kilo 100.

Mkoani Songea bei ya mahindi imeendelea kushuka na kufikia Sh38,000 kutoka Sh40,000 iliyouzwa Septemba 2, 2024. 

Mkoa wa Rukwa unaongoza kwa kuwa na bei za chini za mazao matatu ambayo ni Mchele unaouzwa Sh120,000, Viazi mviringo Sh55,000 na Ngano Sh65,000 kwa kila gunia la kilo 100.

Enable Notifications OK No thanks