Rais Samia: Nimefanya mabadiliko ya kawaida kuboresha ufanisi

August 15, 2024 4:19 pm · Bacley Madyane
Share
Tweet
Copy Link
  • Awataka wateule kuongeza ufanisi katika maeneo yao, kusimamia viapo vyao, na kuishi kwa maadili.
  • Aahidi kukutana nao mmoja mmoja atakaporejea kutoka kwenye mkutano wa SADC.

Dar es salaam. Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema mabadiliko ya uongozi aliyofanya katika nafasi mbalimbali ikiwemo baraza la mawaziri ni ya kawaida kwa ajili ya kuboresha ufanisi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dk. Moses Kusiluka Rais Samia jana Agosti 14, 2024 alifanya mabadiliko kwenye baraza la mawaziri kwa kuteua mawaziri wawili na kuhamisha wengine wawili.

Mabadiliko mengine ni ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Naibu Mwanasheria Mkuu, Jaji wa Mahakama ya Rufani, Wakili Mkuu wa Serikali pamoja na wakuu wa taasisi za umma ikiwemo Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).

Rais Samia aliyekuwa akizungumza katika hafla ya kuwaapisha viongozi aliowateua leo Agosti 15, 2024 Ikulu jijini Dar es Salaam amewataka viongozi hao kwenda kuongeza ufanisi katika maeneo yao, kusimamia viapo vyao, na kuishi kwa maadili.

Mkuu huyo wa nchi, ametumia chini ya dakika tatu kuzungumza na wateule aliowaapisha, akiahidi kuwaita viongozi hao kila sekta kwa ajili ya kuzungumza nao mara atakaporejea nchini kutoka kwenye mkutano wa 44 wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).

“Ninachotaka kusema ni kile alichokisema Makamu wa Rais kwamba kwenye kufanya kazi zenu kuna professionalism (utaalamu) wako uliosomea binafsi lakini kuna kujiongeza kutumia ‘common sense’ (ufahamu wa jumla/kawaida).  Pale unapoona ‘common sense’ inaweza kutumika vizuri tumieni, jiongeze, fanyeni kazi tuwatumikie wananchi,” amesema Rais Samia.

Wanaopewa nafasi ni tatizo

Awali Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma aliyekuwa akizungumza katika hafla hiyo, amesema mapungufu ya sheria, bajeti au taasisi si changamoto zinazozikabili nchi zinazoendelea, bali tatizo ni wanaopewa nafasi za kutekeleza sheria na wale wanaolengwa nazo.

Kwa mujibu wa Profesa Juma, matatizo kwa wanaopewa nafasi hizo yanatokana na wengi wao kuwa na tabia na tamaduni binafsi ambazo hupoteza malengo yanayolengwa na sheria.

“Kwa hiyo tunapokwenda sehemu zetu za kazi, pamoja na kuangalia sheria lakini lazima tuangalie nafsi zetu wenyewe, tuna fikra hasi zozote, tuna tabia ambazo zinafanya sheria zisifanye kazi,” amesema Prof. Juma.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
25 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
25 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
25 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa wananchi kupima afya, kuacha uoga

Rais Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa wananchi kupima afya, kuacha uoga

Nukta TV

Uwepo wa vifaa, madaktari uendane na huduma inayotakiwa

Uwepo wa vifaa, madaktari uendane na huduma inayotakiwa

Nukta TV

Rais Samia: Maradhi ya moyo, saratani kwa watoto yaongezeka Tanzania

Rais Samia: Maradhi ya moyo, saratani kwa watoto yaongezeka Tanzania

Nukta TV