Kimbunga IALY kusababisha mvua, upepo kwa siku mbili Tanzania

May 20, 2024 3:41 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • TMA yasema wakazi wa mikoa ya pwani visiwa vya Unguja, Pemba na Mafia watakumbwa na hali mbaya ya hewa kwa siku mbili.
  • Yawataka wananchi kuchukua tahadhari.

Dar es Salam. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imewatahadharisha wananchi wa mikoa ya ukanda wa pwani na visiwa vya Unguja, Pemba na Mafia juu ya uwepo wa upepo mkali na mvua kubwa zitakazosababishwa na kimbunga IALY kilichopo katika Bahari ya Hindi.

Taarifa ya TMA iliyotolewa leo Mei 20, 2024 saa 11 jioni imesema licha ya kimbunga hicho kuonekana kupungua nguvu wakazi wa mikoa ya Tanga, Lindi, Mtwara, Dar es Salaam, visiwa vya Unguja, Pemba na Mafia watakumbwa na hali mbaya ya hewa kwa siku mbili.

“Matarajio ni kwamba, vipindi vya upepo mkali unaozidi kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayozidi mita 2 vitaendelea kujitokeza katika maeneo ya ukanda wa pwani ya nchi yetu na katika Bahari ya Hindi kati ya leo tarehe 20 Mei 2024 na usiku wa kuamkia Jumatano tarehe 22 Mei 2024 kabla kimbunga IALY hakijaisha nguvu yake kabisa,” imesema taarifa ya TMA.

Taarifa ya TMA imekuja ikiwa ni siku tatu tangu kutangazwa kwa uwepo wa kimbunga hicho nchini Tanzania na maeneo mengine ikiwemo visiwa vya Madagascar na Shelisheli.

Hata hivyo TMA imebainisha kuwa mifumo ya hali ya hewa inaonesha kimbunga hicho kinaelekea upande wa kaskazini mbali na pwani ya Tanzania na kinatarajiwa kuisha nguvu usiku wa kuamkia Mei 22 mwaka huu.

TMA  imewashauri watumiaji wa bahari na wananchi wa maeneo ya ukanda wa pwani kuchukua tahadhari, kuendelea kufuatilia na kuzingatia taarifa za utabiri kutoka mamlaka hiyo pamoja na kupata ushauri na miongozo ya wataalamu wa kisekta.

“TMA inaendelea kufuatilia mwenendo wa kimbunga hicho na athari zake kwa mifumo ya hali ya hewa hapa nchini na itaendelea kutoa taarifa kila inapobidi,” imeongeza taarifa ya TMA.

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Nukta TV

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Nukta TV

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Nukta TV