Serikali yajipanga kuwapandikiza Sokwemtu katika hifadhi za Ibanda na Rumanyika

July 13, 2019 7:54 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Ikolojia ya maeneo hayo inaruhusu kustawi kwa wanyamapori hao kwa kuwa yana makazi mazuri na chakula cha kutosha.
  • Ni hifadhi zilizotangazwa hivi karibuni kuwa hifadhi za Taifa na Rais wa John Magufuli.
  • Hatua hiyo itachochea utalii na ukuaji wa pato la Taifa. 

Dar es Salaam. Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla amesema watawapandikiza Sokwemtu katika hifadhi za Taifa za Rumanyika Orugundu na Ibanda za mkoani Kagera kwa kuwa hifadhi hizo zina mazingira mazuri na chakula cha kutosha kinachoruhusu kustawi kwa wanyamapori hao.

Hatua hiyo itachangia kukuza shughuli za utalii wa Sokwemtu hapa nchini na kuongeza pato la Taifa linalotoka katika sekta ya utalii. 

Taarifa ya Wizara ya Maliasili na Utalii iliyotolewa leo (Julai 13, 2019) imeeleza kuwa Dk Kigwangalla ametoa kauli hiyo mkoani Kagera wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya shughuli za uhifadhi katika hifadhi hizo zilizotangazwa hivi karibuni kuwa hifadhi za Taifa  na Rais John Magufuli.

Hifadhi za Taifa za Rumanyika Orugundu inapatikana wilayani Karagwe ambapo ile ya Ibanda iko Wilaya ya Kyerwa, mkoani Kagera.


Zinazohusiana: 


Waziri huyo amesema mpango huo umekuja kufuatia taarifa za kitaalam kuonyesha kuwa katika miaka mingi iliyopita kulikua na Sokwemtu katika maeneo hayo ya wilaya ya Kyerwa na Karagwe.

Amebainisha kuwa ikolojia ya maeneo hayo inaruhusu kustawi kwa wanyamapori hao kwa kuwa yana makazi mazuri na chakula cha kutosha.Wahifadhi wakiwa na Waziri wa Maliasili na Utalii  ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Rumanyika Orugundu wilayani Karagwe wakati wa ziara ya Kikazi ya Waziri wa Maliasili na Utalii Dk Hamis Kigwangalla katika hifadhi hiyo. Picha| Wizara ya Maliasili na Utalii.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Nukta TV

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

Nukta TV

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Nukta TV