Mkombozi Bank yapata bosi mpya

January 24, 2018 6:43 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link

  • Ni kigogo aliyewahi kufanya kazi katika benki za NMB, Exim na Standard Chartered.
  • Anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Edwina Lupembe aliyestaafu.

Dar es Salaam. Sekta ya benki nchini imempokea bosi mpya, baada ya Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya biashara ya Mkombozi kumteua George Shumbusho kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya kuanzia kuanzia Desemba mosi, 2017.  

Shumbusho, ambaye ni moja ya watu maarufu katika sekta hiyo ya fedha, anachukua nafasi ya iliyoachwa wazi na Edwina Lupembe aliyestaafu Desemba 31 mwaka jana baada ya kuhudumu benki hiyo tangu Agosti 2009.

Edwina alikuwa moja ya vigogo wachache wanawake katika sekta ya benki nchini akiwa sambamba na wenzie kama Ineke Bussemeker wa NMB, Jacqueline Woiso wa Bank M na Mwanahiba Mzee wa Eco Bank.

Taarifa kwa umma iliyotolewa na Menejimenti ya Bodi katika vyombo vya habari leo, Januari 24, 2017 imemshukuru Lupembe kwa kazi yake nzuri ya mfano aliyoifanya katika miaka minane aliyoongoza benki hiyo iliyooanzishwa na Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) mwaka 2009.

“Bodi ina imani kuwa mkurugenzi mpya atatumia uzoefu wake wa kitaaluma kwa kufanya kazi karibu na wafanyakazi wa benki, Bodi na wadau wengine katika kuindeleza benki yetu wakati wa uongozi wake,” inasomeka sehemu ya taarifa hiyo.

Kabla ya uteuzi huo mpya katika benki hiyo inayotoa huduma za mikopo kwa wafanyabiashara wadogo, wa kati na wakubwa, Shumbusho alishawahi zitumikia benki kubwa nchini zikiwemo Exim Bank, Stanbic Bank, Standard Chartered na NMB.

Shumbusho mwenye shahada ya uzamili ya biashara (MBA) kutoka Shule ya Usimamizi wa Biashara ya Maastricht nchini Uholanzi, ni mtaalamu wa masoko na huduma za kibenki.

Kigogo huyo anaingia kuiongoza benki hiyo katika kipindi ambacho sekta ya benki inakabiliwa na changamoto lukuki ikiwemo kuongezeka kwa mikopo chechefu kutoka asilimia 9.1 Septemba 2016 hadi asilimia 12.5 Septemba, 2017, kwa mujibu wa Wizara ya Fedha na Mipango. Mwenendo huo umekuwa ukitishia mustakabali wa benki nyingi nchini hususan zenye mitaji midogo.

Mkombozi Bank ni moja ya benki muhimu kwa ukuzaji wa biashara nchini kutokana na kutoa huduma za mikopo ya vikundi, kilimo, biashara, vifaa na uwekezaji na mikopo inayotokana na dhamana ya mishahara.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
21 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
21 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
21 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Nukta TV

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Nukta TV

FAHAMU KUHUSU SIKOSELI | Part 1: Ugonjwa wa kurithi, unaotesa maelfu ya watoto Tanzania

FAHAMU KUHUSU SIKOSELI | Part 1: Ugonjwa wa kurithi, unaotesa maelfu ya watoto Tanzania

Nukta TV