Vitu adimu vilivyo kwenye Samsung Galaxy Note 9 inayotumia chaja ya ‘wireless’
- Bei ya simu hiyo ya Sh2.3 milioni ni zaidi ya wastani wa kipato cha Mtanzania kwa mwaka.
- Simu hiyo inachajiwa bila kutumia chaja za waya.
- Huenda ikasaidia watu wenye kuhifadhi vitu vingi kwenye simu kutokana na nafasi yake kubwa ya GB 128.
Dar es Salaam. Huenda wewe ni kati ya watu wanaovutiwa na bidhaa mpya zinazoingia sokoni mara kwa mara kutoka kampuni ya vifaa vya kielektroniki ya Samsung. Kampuni hiyo sasa imekuja na simu mpya aina ya Samsung Galaxy Note 9 ambayo hapa Tanzania inatarajiwa kuuzwa si chini ya Sh2,350,000.Â
Toleo hilo lililozinduliwa hivi karibuni nchini Uingereza limekua na unafuu mkubwa kwa watu wanaopata tabu kwenye kuchaji simu kutokana na uwezo wa simu hiyo kupitisha moto kwa kifaa maalumu kisichotumia nyaya. Ili uchaji, Â utatakiwa kutumia kifaa chenye ubapa na kuweka simu yako juu yake ili kupitisha moto kwa haraka (Wireless fast charge).

Samsung Galaxy Note 9 inatajwa kuwa mkombozi wa watumiaji wa simu wasiopenda kuchaji simu na chaja za nyaya.|Picha Samsung Mobile.
Simu hii huenda ikawa mkombozi kwa watu wenye vitu vingi vya kutunza kwenye simu kwa sababu ya uwezo wake mkubwa  kuhifadhi vitu wa hadi GB 128 za simu yenyewe bila kuongeza kadi hifadhi ya nyongeza (Sd card)
Zikiwa na rangi mbili tu za zambarau na rangi ya blue, simu hizo zinakuwa na muonekano mzuri kwa mtumiaji.
Simu hii huenda pia ikawa na unafuu mkubwa kwa watu wenye kufanya kazi kwenye mazingira tofauti kutokana na  uwezo wake wa kuhimili maji, vumbi hata mchanga iwapo ikitokea bahati mbaya imeangushwa katika mazingira yenye hali hizo vikiwemo vimiminika.
Katika usalama, ina njia mbalimbali za kufungua simu ili kutumia, ikihusisha kutumia kidole, kwa kuonyesha uso, kwa neno siri la kawaida, kwa kuchora alama maalum (pattern).Â
Kutokana na baadhi ya Watanzania kuwa na hamu ya simu hiyo, kampuni ya huduma za simu Tigo ilitangaza huduma ya kuagiza simu hizo mapema (Pre-order) ambayo ilimalizika Septemba 6, 2018. Hata hivyo, Nukta ilipojaribu kupata taarifa za kina juu ya idadi ya watu walioagiza mpaka sasa kutoka Tigo, haikuweza kupata majibu ya haraka.
Pamoja na uwezo wa toleo hilo hilo, simu hii haishikiki kwa watu wenye kipato cha chini kutokana  na bei yake kuwa juu ambao bado wanahaha kupata hata huduma za msingi za chakula na malazi. Bei hiyo ya Sh2.3 milioni ni zaidi ya wastani wa kipato cha Mtanzania kwa mwaka kwa mujibu wa takwimu za Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) za mwaka 2017. Mwaka jana NBS inaeleza kuwa wastani wa pato la mtu kwa mwaka nchini lilikuwa ni Sh2,275,600.
Kwa wateja wa kampuni ya Samsung ni wakati muafaka wa kuchangamikia fursa ya kiteknolojia iliyoletwa na kampuni hii ili kupata simu iliyo na ubora na teknolojia ya hali ya juu kwa matumizi ya watu mbalimbali nchini.