SIKU YA CHOO DUNIANI: Safari bado ndefu

November 19, 2018 9:27 pm · Zahara
Share
Tweet
Copy Link
  • Zaidi ya nusu ya kaya nchini hazina vyoo bora jambo linalowaweka wananchi hasa watoto katika hatari ya kukumbwa na magonjwa ya kuambukiza.
  • Watu milioni 892 duniani hawana sehemu maalumu ya kujisaidia wanatumia vyoo vya mtaani, vichakani au sehemu nyingine zilizo karibu na nyumba zao.
  • Wito wa Umoja wa Mataifa ni Serikali kuongeza elimu kwa wananchi kuhusu ujenzi na matumizi bora ya choo.

Dar es Salaam. Wakati ulimwengu ukiadhimisha siku ya choo duniani, zaidi ya nusu ya kaya nchini hazina vyoo bora jambo linalowaweka wananchi hasa watoto katika hatari ya kukumbwa na magonjwa ya kuambukiza kama kuhara na homa za matumbo. 

Kwa mujibu wa takwimu za wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, hadi kufikia Novemba 2017, ni asilimia 40 tu ya kaya zote nchini ndiyo zilikuwa na vyoo bora ambapo ni sawa na kusema kati ya kaya 10 ni 4 tu zina vyoo bora. 

Kimsingi choo bora hujengwa kwa vifaa vya kudumu, huwa na shimo imara, sakafu imara na inayosafishika kirahisi kwa maji. Choo bora hutunza usiri kwa kutumia paa, kuta imara na mlango unaofungika na wenye komeo. Choo hiki huwa na kifaa cha kunawia mikono na sabuni kwa ajili ya kunawa mikono baada ya kukitumia.

Takwimu hizo zinabainisha kuwa, licha ya kaya nyingi kukabiliwa na changamoto ya vyoo bora, ni asilimia 34 tu sawa na kusema kaya 3 kati ya 10 pekee zina vifaa maalum kama maji na sabuni ya kunawia mikono baada ya mtu kumaliza haja.


Zinazohusiana:


Hali hiyo husababisha kinyesi kusambaa katika maeneo mbalimbali ikiwemo katika vyanzo vya maji. Matukio ya mara kwa mara ya magonjwa ya kuhara yanawafanya watu kuwa katika hatari ya kukumbwa na magonjwa mengine ya mlipuko.

Takwimu za Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, zinaonesha kuwa asilimia 60 hadi 80 ya magonjwa yote ambayo watu hutibiwa hospitalini,  yanasababishwa na kutozingatia kanuni za usafi, ikiwemo matumizi ya maji yasiyo salama.

Hata hivyo, siku ya choo duniani ambayo huadhimishwa Novemba 19 kila mwaka kwa mujibu wa kalenda ya Umoja wa Mataifa (UN) ni mahususi katika kutoa hamasa na kuwakumbusha watu juu ya umuhimu wa matumizi ya vyoo safi na bora na kutimiza lengo la sita la Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) ya mwaka 2030 ambalo linasisitiza kuwapatia wananchi maji safi na salama na usafi wa mazingira.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa kupitia mtandao wa World Toilet Day inasema takribani watu bilioni 4.5 ulimwenguni hawana vyoo bora na salama. Huku watu milioni 892 duniani hawana sehemu maalumu ya kujisaidia wanatumia vyoo vya mtaani,  vichakani au sehemu nyingine zilizo karibu na nyumba zao.

Hii ni kwasababu ya kutokuwa na mwamko wa kujenga vyoo au kuwa na mazoea ambayo yameshajengeka na kuona choo hakina umuhimu, jambo linalowafanya watu kujisaidia kwenye vyanzo vya maji na kusababisha uchafunzi wa mazingira. 

Kwa kuona  umuhimu wa kuwepo kwa vyoo bora, Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa afya na mazingira wamekuwa na kampeni za mikoani ili waweze kusaidiana katika kuwapa watu elimu kuhusu matumizi sahihi ya vyoo.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
21 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
21 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Nukta TV

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Nukta TV

FAHAMU KUHUSU SIKOSELI | Part 1: Ugonjwa wa kurithi, unaotesa maelfu ya watoto Tanzania

FAHAMU KUHUSU SIKOSELI | Part 1: Ugonjwa wa kurithi, unaotesa maelfu ya watoto Tanzania

Nukta TV