Taasisi umma zapewa miezi 6 kujiunga na mfumo wa kielektroniki wa mapato

December 14, 2018 10:34 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link

 

Utasaidia kutatua changamoto zilizopo kwenye mfumo uliokuwepo wa ukusanyanji wa fedha za umma. Picha|Tanzaniatoday.


  • Mpaka sasa taasisi 326 zimeunganishwa na GePG Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Tanesco.
  • Kupitia mfumo huo Serikali inaweza kuona makusanyo yote yanayoingia jambo linaloongeza ufanisi wa upatikanaji wa mapato, uwajibikaji na uwazi.
  • Utasaidia kuongeza uwazi na udhibiti wa fedha za umma, kuboresha na kurahisisha namna ya kulipia huduma za umma.
  • Hata hivyo, mfumo huo unatumika na benki 11 tu kati ya benki zaidi ya 50 na kusababisha mkanganyiko kwa wadau.

Dar es Salaam. Taasisi zote za umma ambazo bado hazijajiunga na mfumo wa kielektroniki wa ukusanyaji wa mapato ya Serikali (GePG) zimetakiwa kujiunga na mfumo huo kabla ya Juni 30, 2019 ili kuongeza uwajibikaji, uwazi na ufanisi wa upatikanaji wa mapato serikalini.

Utaratibu wa makusanyo ya mapato kabla ya ujio wa mfumo wa GePG unatajwa kuwa haukua rafiki kwa sababu ilikuwa ni vigumu kuthibitisha malipo na kuwa na foleni ndefu kwenye ofisi za umma zilizosababishwa na zoezi la kufanyiwa tathmini ya malipo ya huduma na uthibitishaji.

Agizo hilo limetolewa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dk Khatib Kazungu wakati wa mkutano wa mwaka wa  wadau wa utumiaji wa mfumo wa GePG Jijini Dodoma ambapo amesema baada ya muda huo kupita hakutokuwa na fedha yoyote ya umma itakayokusanywa nje ya mfumo wa GePG.

“Napenda kusisitiza kuwa ni lazima kutumia mfumo huu kwa kuwa unaongeza ufanisi na uwazi katika ukusanyaji wa fedha za umma. Pia, utaratibu wa matumizi ya GePG unatoa fursa ya kuwa na njia nyingi za kulipia na kuwapa walipaji wa huduma za Serikali utaratibu rafiki wa kufanya malipo,” amesema Dk Kazungu katika taarifa iliyotolewa na kitengo cha mawasiliano cha wizara hiyo.

Ili kukabiliana na changamoto za ukusanyaji wa fedha za umma, Juni 2017 Serikali iliifanyia marekebisho Sheria ya fedha za umma (PFA) ya mwaka 2001 na kuongeza kipengele kinachotaka fedha zote za umma zikusanywe kupitia mfumo huo uitwao kwa Kiingereza “Government e-Payment Gateway”.

Utaratibu wa GePG unaenda sambamba na utekelezaji wa maelekezo mengine ya Serikali yanayohusu makusanyo ikiwemo yale yanayotaka akaunti kuu za makusanyo za taasisi za umma kuwepo Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Kazungu amebainisha kuwa ni lazima kuhakikisha akaunti za taasisi za umma za makusanyo zilizoko  BoT zimewasilishwa kwa Katibu Mkuu wa wizara ya fedha ili ziunganishwe na GePG.

Mpaka sasa takribani benki 11 na mitandao sita ya malipo kwa njia ya simu za kiganjani zimeshaunganishwa na mfumo huo.

Katika kuongeza ufanisi, Dk Kazungu amesema ni vyema taasisi hizo kuwa na akaunti za makusanyo kwenye benki zaidi ya moja kati ya benki zilizounganishwa na GePG ili kuwarahisishia walipaji wa huduma za serikali kwa sababu malipo yote yanayopitia katika mfumo huo hayatozwi ada za miamala na benki hizo.


Zinazohusina: 


Kutekelezwa kwa magizo hayo kutaondoa hatari ya taasisi ya umma kukosa huduma ya malipo endapo benki itashindwa kuzihudumia akaunti zilizounganishwa kwenye mfumo wa GePG.

Mkurungezi wa mifumo ya fedha wa Wizara ya Fedha na Mipango, John Sausi amesema kuwa mfumo huo umekuwa na tija tangu ulipoanzishwa na mpaka sasa taasisi 326 zimeunganishwa na GePG zikiwemo Wakala wa Misitu, Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).

Amezitaja changamoto za Mfumo huo kuwa ni pamoja na Benki 11 tu ndizo zinazotumia mfumo huo kati ya benki zaidi ya 50, hivyo kuleta mkanganyiko kwa wadau wanaotumia  mfumo huo.

Lengo la kuanzishwa kwa GePG ni kutatua changamoto zilizopo kwenye mfumo uliokuwepo wa ukusanyanji wa fedha za umma ili kuongeza uwazi na udhibiti wa fedha za umma, kuboresha na kurahisisha namna ya kulipia huduma za umma.

Pia ni kupunguza gharama zinazoambatana na ukusanyaji wa fedha hizo ambapo mfumo huo ulianza kutumiwa rasmi na taasisi za umma Julai 2017 baada ya majaribio yake kukamilika.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
27 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
27 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
27 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wamiliki wa 'Guest House, Lodge' sajilini kila anayeingia kwa NIDA

Wamiliki wa 'Guest House, Lodge' sajilini kila anayeingia kwa NIDA

Nukta TV

Ndejembi: Watanzania wataanza kuona bei ya mafuta ikishuka

Ndejembi: Watanzania wataanza kuona bei ya mafuta ikishuka

Nukta TV

Katambi asitisha mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa TANZANIA

Katambi asitisha mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa TANZANIA

Nukta TV