‘Infographics’ 10 bora tulizochapisha mwaka 2018
- Waandishi wa nukta.co.tz wamechagua vielelezo mbalimbali vya habari hasa za takwimu ambavyo vilitoa habari zilizojificha na kuwasaidia wasomaji kuelewa mambo kirahisi.
- Ukiachana na changamoto zinazotukabili, kwa timu ya nukta.co.tz, 2018 ulikuwa ni mwaka wa kuishi ndoto ya kutoa habari na makala bora za uchambuzi.
Ni kama jana tu ilikuwa Januari Mosi 2018. Leo tunamaliza mwaka yaani siku 365. Kuna mengi yemafanyika katika maisha yetu: mafanikio lukuki na yenye kutia faraja na yale ya kukatisha tamaa.
Ukiachana na changamoto zinazotukabili, kwa timu ya nukta.co.tz, 2018 ulikuwa ni mwaka wa kuishi ndoto ya kutoa habari na makala bora za uchambuzi kuhusu biashara, uchumi, teknolojia, uvumbuzi kwa ujumla, takwimu, safari na maendeleo.
Licha ya kuwa tumezalisha mamia ya habari na vielelezo vya takwimu (infographics) mwaka huu ambazo kwa namna moja ama nyingine zimesaidia kubadilisha maisha ya watu na biashara zao, waandishi wa Nukta wamechagua infographics 10 bora zilizochapishwa mwaka 2018.
Baadhi ya infographics  hizi ziliandaliwa na wanafunzi waliokuwa katika mafunzo ya uandishi wa habari jambo linalotutia moyo kuwa siku moja uandishi wa habari mtandaoni Tanzania utakuwa ukitawaliwa na vijana wabunifu na wenye shauku ya kubadili tasnia ya habari.
10. Ni kweli ngoma ya Harmonise ‘Kwangwaru’ ni zaidi ya zote?

9. Nani ana hazina kubwa ya wafuasi Twitter Tanzania
​
8. Habari iliyojificha nyuma ya ukuaji wa huduma za posta

7. Fursa zilizopo kwenye uzalishaji wa kakao Tanzania
​
6. Serikali inavyozidi kukaza uzi ukusanyaji wa mapato

5. Ukweli kuhusu uzalishaji wa samaki nchini

4. Tunayoyafahamu kuhusu ajali ya MV Nyerere

3. Kuna mchango wowote wa mazao ya GMO katika kilimo?
2. Sababu zinazofanya ufuatilie mjadala wa bei ya korosho

1. Walimu wa Sayansi ni nusu tu ya mahitaji

Huenda hukufanikiwa kusoma infographics zote tulizozalisha mwaka 2018, lakini je unafikiri zote zilizoainishwa hapa zinafaa kuingia kwenye 10 bora mwaka 2018?
Maoni yako yatasaidia kuboresha kazi zetu mwaka 2019.
Tunakutakia Kheri ya Mwaka Mpya 2019 na endelea kusoma habari za Nukta kwa yanayokuhusu.
Latest