Namna ya kujenga, kuiongezea thamani ‘Personal Brand’ yako
- ‘Personal Brand’ni utambulisho binafsi unaoakisi mwonekano wako wa mavazi, unavyoongea na unavyotenda mambo yako.
- Unapojenga utambulisho binafsi zingatia kusudi lako, kupata maarifa na taarifa sahihi, kuonyesha uwezo wako na kuuza utaalamu wako.
‘Personal Brand’ni utambulisho wako binafsi, ni kile kitu watu wengine wanakizungumza wakati wewe haupo, kwa lugha nyepesi watu wanakujua na kitu gani.Â
Kama watu wengine pembeni yako wanakujua kama wewe ni mpiga kazi, unajitolea, mkarimu, mpole, mtu nadhifu, mwizi. Hii ndiyo personal brand yako.
Watu watazungumza utambulisho wako binafsi katika mambo matatu;cha kwanza mwwonekano wako hasa wa mavazikwani nguo zina nguvu ya wewe kupata heshima kwa watu wengine au wewe kunyimwa heshima kisa tu mavazi uliyovaa.
Jambo la pili niunachokiongea(what you talk),mara nyingi watu wamekuwa wakiongea kuumiza (speaking to wound)au kuongea kuponya (speaking to heal). Je wewe uko upande upi unaongea kuponya au kuumiza?
Mwisho Matendo yako, mara nyingi unaonekana ukifanya nini, mfano mzuri ni mimi mwenyewe nimekuwa nikionekana kwenye televisheni, magazetini, mitandaoni kama hapa Nukta, kwenye majukwaa mbalimbali na kusikika kwenye redioninikifundisha kuhusu’Branding’na ndiyo hapo watu wakaanza kuniita MR BRAND,Â
Hata wewe unakoonekana mara nyingi ndiko brand yako inajengwa kwa nafasi kubwa sana. Kama watu watakuona unashinda mtoni ukivua samaki basi Personal Brand yako ni mvuvi.Â
Soma zaidi:
- Namna huduma kwa wateja inavyoweza kukuza brand ya biashara
- Mambo ya kuzingatia unapoanzisha brand yako ya biashara
Unajengaje utambulisho binafsi?
Katika kujenga personal brand zetu kuna hatua nne za msingi lazima uzipitie katika kufikia hiyo brand unayoitamani na kuiishi ndoto yako;
Tambua kusudi lako (know your purpose)
Kwa kujitambua mimi ni David nina kipaji au kipawa cha kuwa mwalimu mzuri au kuwa mwimbaji bora kabisa ulimwenguni. Hii ni hatua ya msingi na ya kwanza katika kuijenga personal brand yako.
Katikakujijua wewe ni nani itakusaidia sasa kuanzia hapo kuwa na watu wenye kukusogeza mbele kwenye kile unachokitamani kukiishi siku moja.Â
Hatua hii pia itakusaidia kuanza kujiweka sawa kiakili na kimwili kuwa vile ambavyo kusudi lako unataka uwe kama unajiona wewe ni Mchungaji basi unaanza kuwa vile wachungaji walivyo sasa.Â
Kusudi lako la wewe kuishi duniani utaliona wakati ukijichanganya na watu wengine. Picha| K15 Photos.
Tafuta maarifa na taarifa juu ya kusudi lako
Baada ya hatua ya awali ya kujitambua mimi nataka kuwa nani, hatua hii unaenda kulijaza maarifa na ufundi lengo lako kwa kujifunza wewe mwenyewe, kutafuta watu waliofanikiwa kwenye eneo lako, kwenda darasani na kujifunza.
Kujiamini na kujituma kuhakikisha unakuwa na taarifa na maarifa ya kutosha ili uwezo kuwa mwenye tija na mwenye kuleta utofauti kwenye soko la ushindani.
Onyesha uwezo wako
Hiinihatua ya kwenda kwenye soko na kuwaonyesha kuwa mimi ni mwalimu mzuri sana baada ya kulijua kusudi na kulijenga kwamaarifa na taarifa za msingi.Â
Kwa namna gani unaweza kupata nafasi za kuonyesha uwezo wako na utaalamu ni kupitia kujitolea, kuomba kufanya kazi bure. Jambo la msingi hapa ni kupata nafasi au jukwaa la kuuza ulichonacho.Â
Hapa utaweza kuonekana kwa watu na walaji watasema tunahitaji huduma yako na kuanzia hapoutaanza kukua nakuacha mbegu chanya kwa watu wengine juu ya huduma na bidhaa uliyonayo.Â
Wape watu nafasi ya kukusikiliza ili kudhihirisha kipaji na uwezo uliopo ndani yako. Mrejesho watakaoukupa utakusaidia kuboresha zaidi uwezo wako. Picha|K15 Photos.
Uza utaalamu wako
Baada ya hatua ya tatu ya kuonyesha uwezo na utalaamu wako ulionao, sasa uko tayari kusema mimi nitakufundishia watoto kwa kiasi hiki cha pesa kwa sababu watu wanakuamini na wanajua wewe ni nani na unafanya kazi kwenye uwezo upi na hata ukisema ulipwe kiasi fulani cha pesa watu wanakuwa wanajua thamani unayoitoa kwao.Â
Hata hivyo, ili uendelee kufanya vizuri kwenye soko kuna ulazima wa kuendelea kujifunza bila kuchoka, kukua na kupata maarifa na taarifa mpya zaidi.
Charles Nduku maarufu kama Mr Brand ni mkufunzi wa wajasirimali katika masuala ya masoko na uhamasishaji wa kimaisha. Kwa mawasiliano, maoni na ushauri wasiliana naye kupitia +255762918153 au baruapepe mrbrandtz@gmail.com.