Rwanda yaungana na mataifa 50 kusitisha safari za ndege aina ya Boeing 737 Max 8

March 15, 2019 7:38 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Katika taarifa iliyotolewa katika ukurasa wa Twitter wa Shirika la usafiri wa ndege Rwanda (RCAA) inaeleza kuwa marufuku hiyo imeanza mara moja mpaka hapo itakapoamriwa vinginevyo. 
  • Mpaka sasa mataifa zaidi ya 50 yamepiga marufuku matumizi ya ndege hizo.

Rwanda imeungana na nchi nyingine duniani kupiga marufuku kampuni za ndani za ndege na marubani kutotumia ndege za Boeing 737 Max 8 na Max 9 katika anga la nchi hiyo, ikiwa zimepita siku tano tangu ndege kama hiyo ipate ajali katika ardhi ya Ethiopia na kuua watu 157 waliokuwemo ndani.

Mpaka kufikia jana mataifa 50 ikiwemo Marekani, China, Uingereza, India na Australia yalizuia mashirika ya ndani ya ndege katika nchi zao kutumia ndege hizo ikiwa ni hatua ya kuwalinda raia wao na hatari inayoweza kutokea.

Katika taarifa iliyotolewa katika ukurasa wa Twitter wa Shirika la usafiri wa ndege Rwanda (RCAA) inaeleza kuwa marufuku hiyo imeanza mara moja mpaka hapo itakapoamriwa vinginevyo. 

“Shirika la usafiri wa ndege Rwanda kwa uwezo liliopewa katika kifungu cha 16 cha sheria za usafiri wa ndege nchini linaagiza marubani na kampuni za ndege zinazohudumu ndege za Boeing 737 – 8 Max na Boeing 737 – 9 Max, zisiendeshe usafiri wowote wa ndege hizo katika anga ya Rwanda mara moja,” inasomeka taarifa hiyo.

Taarifa kutoka vyombo vya habari vya kimataifa zinaeleza kuwa Rwanda ilikuwa na mpango wa kukodisha ndege mbili aina ya Boeing 737- 800. Huenda mpango huo ikasitishwa kwa muda wakati ikisubiri uchunguzi wa chanzo cha ajali ya ndege ya Ethiopia iliyoanguka Jumapili nje kidogo ya mji mkuu Addis Ababa.


Soma zaidi: Shirika la ndege la Ethiopia limesitisha safari zote za ndege aina ya Boeing 737


Tayari Shirika la ndege la Ethiopia limesafirisha kwenda Paris, Ufaransa kisanduku cha kurekodia kumbukumbu ya mawasiliano ya ndege (black box) ya ndege ya Boeing 737 Max 8 kwa ajili ya uchunguzi ya uchunguzi zaidi.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
21 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
21 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
21 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Nukta TV

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Nukta TV

FAHAMU KUHUSU SIKOSELI | Part 1: Ugonjwa wa kurithi, unaotesa maelfu ya watoto Tanzania

FAHAMU KUHUSU SIKOSELI | Part 1: Ugonjwa wa kurithi, unaotesa maelfu ya watoto Tanzania

Nukta TV