ILO: Watu 7,500 hufariki kila siku duniani wakiwa kazini

April 20, 2019 7:45 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link

Mamlaka za ajira zimeshauriwa kupitia upya mabadiliko ya utendaji wa kazi yanayoruhusu watu wengi kuajiriwa na wakati huo huo wanafanya kazi zinazowaletea shinikizo na hofu ya kupoteza kazi na kuingiliwa kwa faragha zao. Picha|Mtandao.


  • Ripoti mpya iliyotolewa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) imebainisha kuwa vifo hivyo vinasababishwa na mazingira yasiyo salama na afya katika maeneo ya kazi duniani. 
  • Kila mwaka watu zaidi ya 374 milioni wanajeruhiwa au wanaugua kwa sababu ya ajali kazini ikiwemo kufanya kazi muda mrefu bila kupumzika. 
  • ILO yapendekeza tathmini ifanyike kwa sera, teknolojia na matumizi ya mifumo ya kidijitali, maroboti inayotumiwa na wafanyakazi.

Dar es Salaam. Ripoti mpya iliyotolewa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) imebaini kuwa  kila siku watu 7,500 hufariki dunia ulimwenguni kutokana na mazingira yasiyo salama na afya katika maeneo ya kazi, jambo linalopunguza nguvu kazi inayohitajika katika maendeleo ya kiuchumi. 

Pia kila mwaka watu zaidi ya 374 milioni duniani wanajeruhiwa au wanaugua kwa sababu ya ajali kazini ikiwemo kufanya kazi muda mrefu bila kupumzika. 

Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyopewa jina la Usalama na Afya kama Kitovu cha Mustakabali wa  Kazi (Occupational Safety and Health (OSH) imeeleza kuwa mabadiliko ya mazingira ya kazi, teknolojia za kisasa na watu kufanya kazi popote pale na wakati wowote pamoja na ukosefu wa usalama kazini ni sehemu ya mambo yanayosababisha vifo hivyo kila siku duniani.

Katika taarifa yake wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo jana (Aprili 18,2019) New York Marekani, Mtaalam wa ILO kuhusu usalama kazini, Manal Azzi amesema katika mazingira hayo wafanyakazi wanatakiwa kufanya  kazi zaidi na zaidi na hawana muda wa kupumzika hali inayoweza kusababisha magonjwa ya akili, msongo wa mawazo na hata magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama vile saratani na moyo.

“Watu mbalimbali wanafanya kazi kwa njia mbalimbali ikiwemo simu, kompyuta mpakato unazoweza kwenda nazo kila pahali. Intaneti inapatikana kwa kila mtu, simu za kimataifa zinafanya mtu aweze kupatikana wakati wowote,” amesema Azzi katika taarifa hiyo.

Katika mapendekezo ya ripoti hiyo, ILO inaeleza kuwa ili kukabiliana na hali hiyo zinatakiwa ziwepo sera bunifu za ajira zinazojali afya ya umma na kuimarisha sheria za viwango vya kazi kimataifa na kitaifa.

Pia tathmini ifanyike kwa teknolojia na matumizi ya mifumo ya kidijitali, maroboti ambazo zinaweza kuathiri afya ya kisaikolojia ya mfanyakazi kama hazitatumiwa kwa usahihi. 


Soma zaidi:


Mamlaka za ajira zimeshauriwa kupitia upya mabadiliko ya utendaji wa kazi yanayoruhusu watu wengi kuajiriwa na wakati huo huo wanafanya kazi zinazowaletea shinikizo na hofu ya kupoteza kazi na kuingiliwa kwa faragha zao.

Ripoti hiyo imetolewa wakati wadau mbalimbali wa maendeleo wakiwa katika maandalizi ya Siku ya Usalama Kazini itakayofanyika Aprili 28, 2019.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
26 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
27 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
27 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Nukta TV

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Nukta TV

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Nukta TV