Rais Museveni: Nimekuja Tanzania kufanya hija ya historia ya kisiasa

July 13, 2019 12:10 pm · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Amesema hija hiyo ni kukumbuka mchango wa Tanzania uliotolewa wakati wa kupigania huru wa nchi yake.
  • Amesema shida iliyobaki katika nchi hizo mbili ni upatikanaji wa maendeleo, utajiri na kazi. 
  • Rais Magufuli amuhakikishia kuendelea kudumisha uhusiano uliopo baina ya nchi hizo mbili. 

Dar es Salaam. Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amesema amekuja Tanzania kufanya hija ya historia ya kisiasa huku akibainisha changamoto tatu ambazo nchi hizo mbili zitakuwa na kibarua kigumu kuzitatua ikiwemo upatikanaji wa maendeleo.

Museveni aliyekuwa akizungumza leo (Julai 13, 2019) muda mfupi baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Chato mkoani Geita, amesema Tanzania na Uganda zimekuwa na historia ya muda mrefu ya kisiasa ambayo mpaka leo inakumbukwa. 

Amesema Hayati Mwalimu Julius Nyerere aliisaidia sana Uganda kupata uhuru na kuendeleza umoja na mshikamano, kwa hiyo ziara iliyoifanya leo ni kama amekuja kufanya hija ya kisiasa.  

“Kwa hiyo, sababu nimesema nikija hapa nakua kama mtu amekwenda kwenye hija. Nakua nakuja kwenye hija ya kihistoria ya kisiasa,” amesema Rais Museveni. 

Amebainisha kuwa nchi hizo mbili zina amani na utulivu wa kisiasa lakini bado zina changamoto tatu ambazo zinatakiwa ziangaliwe vizuri ili kuhakikisha ustawi mzuri wa wananchi wa nchi hizo mbili za Jumuiya ya Afrika Mashariki.  

“Kwa hiyo changamoto ya leo ni maendeleo pamoja na utajiri na kazi. Bahati nzuri tuko na amani na Tanzania ilichangia kuleta amani Uganda. Uganda iko na amani na Tanzania imekuwa na amani muda mrefu kwa sababu ya uongozi mzuri wa Chama Cha Mapinduzi,” amesema Rais huyo. 

Ili nchi ipige hatua, amesema wananchi wake hawana budi kufahamu tofauti iliyopo katika changamoto tatu cha maendeleo, utajiri na kazi ambazo ndiyo imekuwa shida kubwa barani Afrika.

Amesema maendeleo ni vitu vinavyotumiwa na watu wote kwenye jamii ikiwemo barabara, hospitali na shule ambayo ndiyo kichocheo cha upatikanaji wa utajiri wa mtu mmoja mmoja. 


Zinazohusiana: 


Hata hivyo, amesema utajiri haupatikani kama hakuna kazi zinazotokana na uzalishaji mali na uwekezaji unaofanywa na watu katika sekta ya mbalimbali za maendeleo. 

“Wengine wanasema mambo ya kazi. Kazi inatokana na mali, kama nikijenga hoteli, kama mtu binafsi nakuja hapa Chato najenga hoteli ni yangu binafsi, huo ni utajiri wangu unazaa kazi za Watanzania na Waganda,” amesisitiza Rais Museveni. 

Katika hatua nyingine, amesema Uganda itaendelea kuimarisha uhusiano wake na Tanzania hasa kupitia ujenzi wa bomba la mafuta toka Hoima hadi Tanga, ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR na uwanja wa ndege wa Chato ambao uko karibu zaidi na jiji la Entebe.

Rais Museveni yuko nchini kwa ziara ya siku moja akitokea nchini Angola ambapo ametua moja kwa moja katika uwanja wa ndege wa Chato na anafanya mazungumzo na Mwenyeji wake Rais John Magufuli katika kijiji cha Mlimani wilayani humo.

Rais John Magufuli (kushoto) akiwa na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni katika maja ya matukio yaliyofanyika kipindi cha nyuma. Picha|Mtandao. 

Kwa upande wake, Rais John Magufuli wakati akimpokea mgeni wake, amesema Tanzania na Uganda zina historia ya muda mrefu ya undugu na ujirani mwema ambayo itazidi kuimarishwa na kuendelezwa.  

“Kwetu sisi Watanzania, Mhe. Museveni tunakuona ni ndugu yetu ni ndugu yetu wa kweli,” amesema Rais Magufuli.

Kutokana na uhusiano huo, kwa mujibu wa Rais Magufuli, biashara kati ya Tanzania na Uganda mwaka 2018 ilifikia Sh358.697 bilioni kutoka Sh178.191 bilioni mwaka 2015.

“Aidha Uganda ina miradi ipatayo 22 ya uwekezaji nchini yenye thamani ya dola za Marekani milioni 143.25 ambayo imetoa ajira ya watu wapatao 2,230,” amesema. 

Hata hivyo, amesema takwimu hizo ni ndogo, jitihada zinahitajika kukuza biashara baina ya nchi hizo mbili kadiri uchumi unavyozidi kupanda. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
21 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
21 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
21 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Nukta TV

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Nukta TV

FAHAMU KUHUSU SIKOSELI | Part 1: Ugonjwa wa kurithi, unaotesa maelfu ya watoto Tanzania

FAHAMU KUHUSU SIKOSELI | Part 1: Ugonjwa wa kurithi, unaotesa maelfu ya watoto Tanzania

Nukta TV