Rais Magufuli akipigia chapuo tena Kiswahili mkutano wa SADC

August 17, 2019 7:22 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Amewaomba wakuu wa nchi za Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) kutoa hutuba yake kwa Kiswahili. 
  • Amesema hotuba hiyo itawashawishi kuridhia Kiswahili kuwa lugha rasmi ya SADC.
  • Amesema ni fahari kubwa kwa Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano wa SADC.

Dar es Salaam. Rais John Magufuli amewaomba Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) kuridhia na kupitisha Kiswahili kuwa lugha rasmi ya nne itakayokua inatumiwa katika shughuli mbalimbali za jumuiya hiyo. 

Agosti 14, 2019, Lugha ya Kiswahili ilipendekezwa na Baraza la Mawaziri la SADC kuwa lugha rasmi  ya nne itakayotumiwa katika shughuli za mawasiliano katika jumuiya hiyo.

Iwapo kitapitishwa na Wakuu wa nchi za SADC katika mkutano unaofanyika leo na kesho, Kiswahili kitaungana na lugha za Kifaransa, Kiengereza na Kireno zinazotumika katika shughuli rasmi za jumuiya hiyo.  

Rais Magufuli aliyekua akizungumza leo (Agosti 17, 2019) wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wakuu wa nchi za SADC jijini Dar es Salaam, amesema amewaomba wageni walioshiriki mkutano huo kutoa hutuba yake kwa Kiswahili. 

Amesema anaamini hotuba yake ya Kiswahili itawashawishi wakuu wa nchi za SADC kuridhia iwe lugha rasmi ya nne ya mawasiliano katika shughuli za jumuiya hiyo yenye nchi 16. 

“Ninawaomba wakuu wa nchi mniruhusu nitoe hutuba yangu ya ufunguzi kwa lugha ya Kiswahili. Kwa kufanya hivyo mtashawishika kukubali na kukipitisha Kiswahili kuwa lugha rasmi ya SADC,” amesema Rais Magufuli. 


Soma zaidi: 


Amesema Kiswahili kinazungumzwa katika nchi 34 za Afrika na sita za SADC, ambapo imekua lugha inayokua kwa haraka duniani. 

Katika hatua nyingine, Rais amesema Tanzania inajisikia fahari kubwa kuwa mwenyeji wa mkutano huo ambao utaikabidhi nchi hiyo ya Afrika Mashariki uenyekiti ambao utadumu kwa miaka miwili ijayo. Tanzania itakabidhiwa uenyekiti kutoka kwa Namibia. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
23 Sep, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
23 Sep, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
23 Sep, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MAMA FATMA KARUME: Sikuolewa na Rais, niliolewa na kiongozi

MAMA FATMA KARUME: Sikuolewa na Rais, niliolewa na kiongozi

Nukta TV

Mama Fatma Karume, kuzikwa leo Septemba 22, 2026 saa 10 alasiri

Mama Fatma Karume, kuzikwa leo Septemba 22, 2026 saa 10 alasiri

Nukta TV

HUU HAPA mwenendo wa ujenzi wa Mradi wa Gesi Asilia Kimiminika (LNG) Lindi

HUU HAPA mwenendo wa ujenzi wa Mradi wa Gesi Asilia Kimiminika (LNG) Lindi

Nukta TV