Magufuli asaini sheria nne zilizopitishwa bungeni

October 1, 2019 7:57 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Sheria hizo ni pamoja na Sheria ya Serikali Mtandao namba 10 ya mwaka 2019.
  • Zilipitishwa katika katika mkutano wa 16 wa Bunge la Tanzania Septemba mwaka huu. 
  • Sheria zilizosainiwa zimetangazwa kwenye gazeti la Serikali na zitapatikana kwenye tovuti ya Bunge.

Dar es Salaam. Rais John Magufuli amesaini sheria nne ikiwemo ya  Sheria ya Serikali Mtandao namba 10 ya mwaka 2019 zilizopitishwa katika mkutano wa 16 wa Bunge la Tanzania  ili zianze kutumika rasmi.

Mkutano huo uliofanyika Septemba mwaka huu pamoja na mambo mengine ulipitisha sheria hizo ili zitumike katika shughuli mbalimbali za utawala. 

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Bunge leo (Octoba 1 2019)inaeleza kuwa sheria hizo zilizosainiwa na Rais, zimetangazwa katika gazeti la Serikali.

Sheria hizo ni pamoja na Sheria ya Serikali Mtandao Na. 10 ya mwaka 2019 ambayo inalenga kusimamia kuwepo kwa uthabiti wa kisheria utakaozuia urudufu wa mifumo na miundombinu ya Serikali mtandaoni.


Zinazohusiana


Nyingine ni Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 4), Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 5) pamoja na Sheria ya marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 6) zote za mwaka 2019.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
26 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
26 May, 2026
No active movers today
Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

Nukta TV

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

Nukta TV

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

Nukta TV