Watanzania wakumbushwa jukumu la kuwalinda, kuwajali wazee

October 1, 2019 3:23 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Wametakiwa kutokwepa jukumu la kuwatunza wazee kwani nguvu zao za uzalishaji mali zimepungua.
  • Jamii imetakiwa kuimarisha upatikanaji wa fursa, haki na ustawi wa wazee ikiwemo kuondokana kabisa na vitendo vya ukatili dhidi yao. 
  • Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, inaonyesha kuwa Tanzania inakadiriwa kuwa na wazee milioni 2.5 sawa na asilimia 5.6 ya wananchi wote.

Dar es Salaam. Ikiwa leo ni maadhimisho ya siku ya wazee duniani, Serikali na wadau mbalimbali wameitaka jamii kutokwepa jukumu la kuwatunza wazee kwani nguvu zao za uzalishaji mali zimepungua.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliyekuwa akizungumza leo (Oktoba 1, 2019) katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wazee Duniani yaliyofanyika Kitaifa mkoani Mtwara. amesema Serikali inaendelea kutekeleza Mkakati wa Kitaifa wa Kutokomeza Mauaji ya Wazee uliozinduliwa Januari, 2019 ili  kutokomeza ukatili kwa wazee ifikapo 2023 na kuhakikisha wazee na watu wenye ulemavu wanatambuliwa na kulindwa dhidi ya ubaguzi, uonevu, ukatili na mila potofu.

Amesema wajibu wa kuwahudumia au kuwasaidia wazeeni ni wa kila mmoja na inatakiwa kila mmoja atambue kwamba wazee hao wamelitumikia Taifa kwa muda mrefu tena kwa namna mbalimbali ikiwemo kuleta mafanikio ambayo jamii inajivunia sasa.

Sambamba na hayo, Majaliwa ametoa rai kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa, wananchi na wadau mbalimbali kuendelea kuimarisha upatikanaji wa fursa, haki na ustawi wa wazee ikiwemo kuondokana kabisa na vitendo vya ukatili dhidi yao. 

“Vituo vyote vya kutoa huduma za afya vya umma kutoa huduma bora na za haraka kwa wazee wetu wenye vitambulisho. Tengeni dirisha maalumu kwa ajili ya kuwahudumia ili wasikae kwenye foleni muda mrefu. Serikali itaendelea kuweka miundombinu na mazingira rafiki ili kuwawezesha kupata mahitaji yao.” amesema Majaliwa.

Maadhimisho ya siku ya wazee duniani hufanyika Oktoba 1 kila mwaka ili kutathmini hatua zilizopigwa katika kuwalinda na kuwatunza wazee dhidi ya vitendo vya ukatili na kuhakikisha wanapata haki zao bila kubaguliwa. 


Soma zaidi: Maoni: 


Nalo shirika la Umoja wa Mataifa (UN) limetoa wito kwa kila mtu kusimama kidete kwa ajili ya kuhakikisha haki za wazee zinatimizwa.

UN imesema, kati ya changamoto zinazokumba mustakabari wa haki za wazee ni pamoja na kukosekana kwa chombo maalum cha kisheria kwa ajili ya wazee.

Kwa upande wake Shirika la Helpage ambalo linalojihusisha na haki za wazee nchini Tanznaia nalo limetoa wito na kuziomba mamlaka kuchua hatua dhidi ya unyanyapaa unaofanywa dhidi ya wazee.

Smart Daniel ambaye ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika hilo amesema maadhimisho hayo kwa mwaka 2019 yamekuja muda mwafaka kwani Serikali ya Tanzania imefanya mambo makubwa kwa ajili ya kusaidia kundi hilo ambalo mara kwa mara linakutana na changamoto nyingi ikiwemo kubaguliwa na unyanyapaa.

“Mapema mwaka huu tulishuhudia kuzinduliwa kwa Mkakati wa Kitaifa wa Kutokomeza Mauaji ya Wazee. Hivi karibuni pia, Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein amekubali kuongeza kiasi cha pensheni jamii ambayo kwa sasa ni Sh20,000” amesema Daniel katika taarifa yake iliyotolewa leo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikabidhiwa zawadi ya kiti cha wazee na Mwenyekiti wa Mtandao wa Wazee Tanzania, Abdallah Majumba  (kushoto) baada ya kuhutubia katika Maadhiisho ya Siku ya Wazee Duniani yaliyofanyika kitaifa kwenye Uwanja wa Nangwada Sijaona mjini Mtwara, Oktoba 1, 2019. Katikati ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu. Picha|Ofisi ya Waziri Mkuu.

Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, inaonyesha kuwa Tanzania inakadiriwa kuwa na wazee milioni 2.5 sawa na asilimia 5.6 ya wananchi wote.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kupitia maadhimisho hayo jamii inakumbushwa kuzingatia na kutekeleza kwa umuhimu haki za wazee na wazee nao wanakumbushwa wajibu wao kwa jamii.

Waziri huyo amesema hadi Desemba 2018 wazee milioni 1.8 wametambuliwa na kati yao wazee 684,383 sawa na asilimia 37 ya wasiokuwa na uwezo wamepatiwa vitambulisho vinavyowawezesha kupata huduma za matibabu bila ya malipo.

 Idadi hiyo ni sawa na ongezeko la asilimia 319 au mara tatu zaidi ya idadi ya wazee 214,370 waliopewa vitambulisho vya matibabu mwaka 2016/2017.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
26 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
26 May, 2026
No active movers today
Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

Nukta TV

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

Nukta TV

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

Nukta TV