Jocker: Filamu itakayokupa sababu za wachekeshaji kukosa furaha inayodumu

October 4, 2019 8:58 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link

Kuonewa na kutengwa na jamii inayomzunguka, kunafanya filamu hii iliyogharimu Sh126 bilioni kuwasilisha kisa cha Fleck ambaye anakuwa kiongozi wa wahalifu wengi wanaojificha nyuma ya kifunika uso (mask) kwenye jiji la Gotham. Picha|Mtandao.


  • Inasimulia maisha ya Arthur Fleck (Joaquin Phoenix) baada ya kutengwa na jamii
  • Jifunze madhara ya upweke na umuhimu wa marafiki.
  • Kwa Sh126 bilioni, mkasa wa Jokeri aliyepoteza mwelekeo unasimamiwa na Todd phillips.

Dar es Salaam. Mazoea ya mfuatilia vichekesho (Comedy) ni kumuona jokeri akichekesha. 

Lakini mambo siyo mambo kwenye filamu ya “Joker” ambayo imeingia kwenye kumbi za sinema leo (Oktoba 4, 2019) kwani filamu hiyo siyo tu inabadilisha taswira ya jokeri (Joker) inakufanya ufikiri mara mbili kila umuonapo mchekeshaji yeyote.

Wengi husema kati ya watu wasio na furaha duniani ni wale wanaowapa furaha wenzao. Msemo huu umetia nanga kwenye filamu hii kwani Arthur Fleck (Joaquin Phoenix) ambaye ni mchekeshaji aliyeshindwa kuendeleza malengo yake anageuka kuwa mhalifu.

Kuonewa na kutengwa na jamii inayomzunguka, kunafanya filamu hii iliyogharimu Sh126 bilioni kuwasilisha kisa cha Fleck ambaye anakuwa kiongozi wa wahalifu wengi wanaojificha nyuma ya kifunika uso (mask) kwenye jiji la Gotham.

Jifunze jinsi upweke na kutengwa kunaweza kukusababishia uendawazimu na hata kufanya “U turn” katika maisha yako.


Zinazohusiana


Kama umewahi sikia msemo wa “good guy gone bad”, tembelea Mlimani City, Mkuki House, Aura Mall na kumbi yeyote ya filamu kuwaona Zazie Beetz (Dead pool, Atlanta na Geostorm), Robert De Niro ( The Irish man na Good Fellas), Frances Conroy (Cat woman) na wengine wengi  wakikuonyesha nini maana halisi ya msemo huo.

Unakosaje filamu iliyoongozwa na kiongozi Todd Phillips aliyekonga nyoyo za mashabiki wake katika filamu za A star is born, The Hangover  (Sehemu ya1, 2 &3), na hata War Dogs.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Nukta TV

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Nukta TV

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Nukta TV