Janga lililojificha nyuma ya matumizi ya “earphones” kwa vijana Tanzania
- Ni kutokana na kushamiri kwa teknolojia ya “earphones” katika kusikiliza muziki na redio.
- Vifaa hivyo vimekuwa chanzo cha ajali, matatizo ya kusikia, vifo na kuzorota kwa mahusiano ya watu kwenye jamii.
- Serikali, wadau washauri watumiaji kutumia kwa kiasi ili kujiweka salama.
Dar es Saaam. Teknolojia ya Earphones (spika za masikioni) imepata umaarufu mkubwa kwa vijana huku wengi wao wakitumia kusikiliza muziki na redio mahali popote walipo kwa kutumia simu au redio.
Hata hivyo, teknolojia hiyo ina madhara yake ikiwa haitatumika kama ilivyokusudiwa kwa sababu inaweza kusababisha magonjwa na hata kifo kutegemeana na mazingira inapotumika.
Earphones ziligunduliwa na Nathaniel Baldwin mwaka 1910 na hutumika kusikilizia muziki na redio pale zinapounganishwa na simu au redio ama kifaa chochote cha kielektroniki chenye kuruhusu matumizi yake.
Baldwin ambaye alizigundua zikiwa na waya, hakuzuia maboresho ya teknolojia hiyo kwani hadi sasa, zipo earphone ambazo ni ndogo zinazoweza kufaliwa kirahisi masikioni.
Lakini zipo zisizotumia waya zinajulikana (Wareless earphone). Yote hiyo ni wabunifu kuwapatia watumiaji kila wanachopenda.
Earphones zaleta gumza mtaani
Licha ya kujipatia wapenzi wengi, teknolojia hiii mekuwa gumzo kwenye shughuli za kila siku yaani majumbani, barabarani na hata maofisini na kuleta sintofahamu ambazo wakati mwingine zimekuwa ni kero kwa watu wasiotumia.
Baadhi ya watu wanashindwa kupeana hata salamu wakiwa kwenye vyombo vya usafiri kwa sababu kila mtu anaendelea na kuchati na simu yake na kupoteza ile maana ya undugu na urafiki.
“Nimeingia kwenye daladala nimesalimia mtu kanikaushia. Tumefika maeneo ya Kivulini (, konda anaita kituo mtu yuko kimya. Ile gari linapitiliza kituo, mtu ndiyo anasema konda shusha kuhamaki anatoa vidude masikioni ndiyo kushangaa kumbe ni headphone (earbuds),” anasema Tekla Mallya, mkazi wa Jijini Dar es Salaam.
Huenda watumiaji wakamjibu Mallya na methali isemayo “Hali ya mtu haijui mtu, mwenye hali kaijulia” kwa sababu watumiaji wa earphones wanasema “ni rahisi mtu kulaumu endapo hajawahi kutuzimia.
Mkazi wa Dodoma, Pious Funzo ni mdau wa spika za masikioni, yeye anasema kila tolea la vifaa hivyo vinapotoka, lazima anunue ili kupata ladha za muziki ambao umekuwa ukimuondolea msongo wa mawazo ya maisha.
“Binafsi nikivaa earphones ninajitenga na ulimwengu wote. Kuna wakati nakuwa nimechoka kusikia ya walimwengu na ninachokitaka ni muziki mzuri pekee. Sitaki kusumbuliwa kabisa,” amesema Funzo.
Teknolojia hiyo ina madhara yake ikiwa haitatumika kama ilivyokusudiwa kwa sababu inaweza kusababisha magonjwa na hata kifo kutegemeana na mazingira inapotumika. Picha|Mtandao.
Hatari iliyojificha nyuma ya vifaa hivyo
Licha ya kuwa vifaa hivyo ni muhimu kwa watumiaji lakini vimekuwa chanzo cha matatizo mengi ikiwemo ajali za barabarani, kukosa umakini, kupunguza ukaribu na watu wengine na kuchangia kupata matatizo ya kutosikia vizuri.
Funzo anasema wakati mwingine wakati anatumia earphones amekuwa anashindwa kuwajibu watu wanaomuongeleshwa kwa sababu hawasikii, jambo ambalo limekuwa likiwafanya watu hao waone kama wanadharauliwa.
“Vitu kama hivyo hunitokea. Kuna muda nashtukia gari lipo nyuma yangu na wengine hunisema kuwa wananiongelesha nashindwa kuwajibu huku wengine wakiniita bila mafanikio,” amesema.
Kadhia hiyo ya watumiaji pia inawapata madereva barabarani, kwani wanapata wakati mgumu kuokoa maisha ya watembea kwa miguu ambao pasipo kujali wanatumia earphone wakiwa wanatumia barabara.
Watu hao hukosa umakini wa kuzingatia kanuni za barabarani kwa sababu vifaa hivyo huwatenga kwa sehemu na yanayoendelea duniani.
“Wapo wanaotumia earphones kuzidi. Kuna watu wanaolala na earphone na wanao amka tu na kuweka earphone masikioni,” anasema Feruzi, mkazi wa Dar es Salaam anayemiliki gari.
Feruzi anasema hauwezi kuisha mwezi bila kupata mkasa na mtu anayetumia barabara huku akiwa na earphone masikioni.
Zinazohusiana
- Michael Tumaini: Mwanafunzi wa shule ya kata aliyetengeneza ‘AC’, Power Bank ya simu
- Mambo ya kuzingatia unapotumia Uber, Taxify
Tabia ya kutumia vifaa hivyo pia imewakumba madereva wa bodaboda, jambo linalowaweka zaidi katika hatari ya kusababisha na kupata ajali. “Akiwa anaendesha anaangalia mbele tu. Pembeni haoni, nyuma ikipigwa honi hasikii. Ukija kushtuka, ajali,” anasema dereva wa bodaboda maeneo ya Victoria, Dar es Salaam, Wilbard Yasinto.
Ripoti ya Shirika la Afya Duniani (WHO) ya Ajali za Barabarani ya mwaka 2017 zinaonyesha kuwa watu milioni 1.25 hufariki kwa ajali kila mwaka ambapo watu milioni 20 hadi milioni 50 hubaki na majeraha na ulemavu wa aina mbalimbali.
Ripoti hiyo inaeleza kuwa nusu ya wanaokufa katika ajali za barabarani zinazotokea duniani kote ni watembea kwa miguu, madereva wa bodaboda na madereva wa magari na kuaathiri asilimia tatu ya pato la ndani la taifa kila mwaka.
Hata hivyo, ripoti hiyo inaeleza kuwa ajali na vifo hivyo vingeweza kuzuilika endapo watu wangezingatia sheria ikiwemo kuvaa kofia ngumu na kuepuka tabia hatarishi ikiwemo kutumia simu, kusikiliza redio kwa njia ya earphone wakati wanatumia barabara.
Nini kifanyike kukabiliana na hali hiyo?
Akitoa suluhu, Feruzi amesema kutokana na matumizi ya teknolojia hiyo wakati mwingine huuchosha ubongo, inahitajika mtu kuzipumzisha earphone zake na kupata muda wa kufanya mambo mengine.
“Mimi ninafanya mazoezi ya kukimbia. Nikiwa nafanya hivyo, ninavaa earphone sikio moja na kuacha lingine kwa ajili ya kusikia yanayoendelea.
Ninajifunza kutumia baadhi ya muda wangu kutoka nje na kufikira mambo mawili matatu kuacha akili yangu ifikiri,” anasema Feruzi ambaye ni mtaalam wa programu za kompyuta.

Mwanamuziki wa nyimbo za injili, Orepa Feruzi anasema njia ya kupunguza athari za earphones, ni mtumiaji kusikiliza kwa sauti ya wastani au ya chini ili kumpa nafasi ya kuelewana na watu wengine.
“Kuna wakati nilipata shida ya kusikia, nilikuwa nasikiliza muziki kwa earphones kwa sauti ya asilimia 100,” anasema Orepa na kuongeza kuwa zipo simu zinazoonya pale mtu ongezapo sauti kubwa.
Earphones haziathiri tu ubongo na umakini barabarani, bali inaweza kuwa chanzo cha matatizo ya kusikia ikiwa zitatumiwa kupita kawaida.
Dk Joshua Sultan ambaye ni daktari wa mafunzo kutoka Chuo cha Tiba na Sayansi Shirikishi Moshi (KCMC) anasema mfumo wa usikilizaji unatakiwa kuanza kwenye sikio la nje na kisha kuingia kwenye sikio la kati na kisha sikio la ndani.
Kwa kutumia earphones, mfumo wa usikilizaji unaanzia sikio la kati, na hivyo zinachosha ngoma ya sikio kwani ngoma ya sikio ina uwezo wake wa kung’amua masafa (frequency) za sauti na pale zinapozidi, ndipo kuchoka kwake kunaanza.
Ili kuwa salama, Sultan amesema unaponunua earphone, zingatia ubora na zile zinazoweza kuchuuja sauti kufikia uwezo wa kutokuwa na madhara makubwa kwenye sikio.
Machi 3, 2019, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ilionya juu ya matumizi ya vifaa hivyo kwa muda mrefu vinasababisha tatizo la usikivu na kulisababishia
Latest
