“The wedding year”: Filamu ya mapenzi iliyojaa visa vya kuchekesha

October 25, 2019 1:48 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Inazungumzia mahusiano ya ndoa na  jinsi ya kuishi na mpenzi wako.
  • Imeja visa vingi ambavyo vitakufundisha nini maana ya ndoa. 

Dar es Salaam. Wiki hii, unahitaji kusahau visu, bunduki na kuachana na michezo ya kareti na kurusha mateke. 

Badala yake, andaa kitambaa kwa ajili ya kujiziba mdomo pale unapocheka na kufuta machozi wakati filamu ya The wedding year itakapokuwa inaonyeshwa katika kumbi mbalimbali kuanzia ijumaa ya leo Oktoba 25.

Filamu hii huenda ikawafaa walio na wanaotarajia kuingia kwenye ndoa,kwa sababu ina visa vingi vitakavyokupa funzo lililotukuka.

Sarah Hayland (Modern Family) hana mpango wa kuingia kwenye ndoa. Na wala hajioni kama msichana aliye tayari kutulizana kwenye mahusiano. Anapompata kijana  Jake Riddick (let it shine) ambaye yuko tayari kuipanda milima na hata kuvuka bahari kwa mbizi kwa ajili yake, mambo yanaanza kutindinganyika.


Zinazohusiana


Mialiko 15 ya kuhudhuria harusi za jamaa zake ndani ya mwaka mmoja, hotuba kwenye harusi za marafiki na dada zake ni vionjo tu ambavyo utakutana navyo kwenye filamu hiyo lakini angalia usiondolewe kwenye kumbi kwa kushindwa kujizuia kucheka.

Tembelea Mlimani City, Aura mall na Mkuki house kujionea filamu hii iliyoongozwa na Robert Luketic ambaye pia ni kichwa nyuma ya kazi kama Monster in Law na Legally Blonde.

/
No matches found for this filter
31 May, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
31 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
31 May, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

Nukta TV

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

Nukta TV

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

Nukta TV