Soko la Soni: Kivutio kingine cha utalii wilayani Lushoto

November 29, 2019 4:21 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Soko hilo lilipo kata ya Soni ni maarufu kwa bidhaa mbalimbali ikiwemo matunda na mboga mboga. 
  • Wageni wanaotembelea Wilaya hiyo huvutiwa zaidi kupita katika soko hilo ili kujipatia bidhaa mbalimbali. 

Dar es Salaam. Utalii siyo tu kutembelea mbuga za wanyama au fukwe za bahari na mito, ni zaidi ya hapo. Hata kutembelea miji ambayo hujawahi kufika nao ni utalii, kwa sababu unakutana na vitu vipya ambavyo huenda haviko kwenye eneo unaloishi. 

Hivi karibuni timu ya www.nukta.co.tz na kampuni ya K15 Photos tulitembelea Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga. Huko tulijionea mengi ikiwemo mandhari nzuri ya wilaya hiyo ambayo imepambwa kwa milima na mabonde yenye miti mizuri na hali ya hewa ya baridi kiasi. 

Katika shughuli zetu, hatukuacha kupita katika Soko la Soni lilipo katika kata ya Soni katika mji huo unaokua kwa kasi Tanzania. Lakini soko hilo liko karibu kabisa na stendi ya mabasi ya Wilaya ya Lushoto, jambo linalofanya watu wengi wavutike kupitia sokoni hapo wawapo safarini. 

Soko hilo limesheheni bidhaa mbalimbali ikiwemo vyakula na matunda ambayo ni muhimu kwa afya yako. Wakulima kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya hiyo wamekuwa wakileta bidhaa katika soko hilo ili kujipatia wateja wanaotoka katika maeneo mbalimbali nchini.  

Hizi ni baadhi ya picha ambazo huenda zikakuvutia siku moja kutembelea soko hilo maarufu lilipo Lushoto. 

Limesheheni matunda na mbogamboga mbalimbali

Kwa wapenzi wa ndizi mbivu basi, maparachichi basi ukifika Lushoto usikose kutembelea soko la Soni. Picha|K15 Photos.

Afya inajengwa kwa matunda kama matango, maparachichi, maembe; pilipili hoho na hata nyanya. Picha|K15 Photos.

Kwa maharage na matango, soko la Soni halitakuacha utoke mikono mitupu ni lazima tu utaacha pesa yako kwa wauzaji ili nao wafaidike na biashara zao. Picha|K15 Photos.

Samaki nao wamejaa tele

Wataalam wa afya wanashauri tule samaki ili kujipatia protini na madini muhimu kwa ajili ya miili yetu. Unaachaje kununua samaki uwapendao ukifika soko la Soni, Lushoto. 

Wakina mama wanatumia fursa ya kuuza samaki ili kujipatia kipato kwa ajili ya familia zao. Picha|K15 Photos.

Kwa wapenzi wa samaki aina ya kambale waliokaushwa vizuri, hiyo nayo ni fursa ya kuinua maisha ya akina mama wa soko hilo. Picha| K15 Photos. 

Wanawake, vijana hawajabaki nyuma

Kutokana soko hilo kuwa karibu na stendi na barabara, vijana na wanawake huwafuata wateja hadi kwenye magari ili kuhakikisha hawaondoki Lushoto bila kununua bidhaa za Wilaya hiyo.

 Ndizi zinawafuata hadi kwenye magari ili kuboresha afya zao. Picha|K15 Photos.

Vijana nao wamesema hawabaki nyumbani, kila siku lazima waende soko la Soni kufanya kazi mbalimbali ikiwemo kubeba mizigo na kuuza bidhaa ili kujipatia kipato. Picha|K15 Photos. 

Una mpango wa kwenda Lushoto? basi usisite kupitia soko la Soni ili ukasafishe macho na kujipatia kile unachopenda. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
17 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
17 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Msemaji Geita: Vijana msikurupuke kuja Katoro

Msemaji Geita: Vijana msikurupuke kuja Katoro

Nukta TV

Magonjwa haya matano yanayoongoza kwa kuua watu duniani

Magonjwa haya matano yanayoongoza kwa kuua watu duniani

Nukta TV

Mambo yakuzingatia kabla ujawasha gari lako asubuhi

Mambo yakuzingatia kabla ujawasha gari lako asubuhi

Nukta TV