Teknolojia, suluhu za asili kuokoa kilimo 2020

December 13, 2019 4:14 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link

Udhibiti endelevu wa maliasili na kulinda bayoanuai kwa ajili ya kufikia mifumo endelevu ya chakula ni muhimu katika kuboresha kilimo na uzalishaji wa chakula. Picha| Erwan Hesry/Unsplash.


  • Ni njia muhimu katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
  • Suluhu za asili zinajumuisha hatua katika mifumo ya udongo, maji, mifugo, bahari na mifumo ya chakula.
  • FAO yasema azma hiyo itafanikiwa ikiwa ushirikiano wa wadau wote  utahimizwa.

Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limesema suluhu za asili za mabadiliko ya tabianchi ikiwemo utunzaji wa misitu ni muhimu na lazima zijumuishe teknolojia ili kuchagiza mifumo bora ya upatikanaji wa chakula.

Mkurugenzi Mkuu wa FAO, Qu Dongyu akizungumza kando ya mkutano wa 25 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi (COP25) mjini Madrid, Hispania,  amesema ubunifu ikiwemo kujumuisha teknolojia kwa sasa ni kitovu cha maendeleo endelevu ya sekta ya kilimo.

Katika taarifa iliyotolewa na FAO, Dongyu amezitaja suluhu hizo kuwa zinajumuisha hatua katika masuala ya misitu na mifumo mingine kama udongo, maji, mifugo, bahari na mifumo ya chakula pamoja na mazingira ya chakula na watumiaji.

“Tunajiandaa kubadili mfumo wa chakula, ni lazima tuufanyie mabadiliko mnyororo wa uzalishaji chakula, thamani na wa usambazaji, suluhu pekee ni ubunifu,” amesema Dongyu wakati.

Amesema azma hiyo itafanikiwa ikiwa ushirikiano wa wadau wote  utahimizwa, jambo likalosaidia kuboresha sekta kilimo mwaka 2020.


Zinazohusiana:


Amesisitiza kuwa udhibiti endelevu wa maliasili na kulinda bayoanuai kwa ajili ya kufikia mifumo endelevu ya chakula ni muhimu katika kuboresha kilimo na uzalishaji wa chakula.

Ametoa mfano wa mradi uliotangazwa mapema jana (Desemba 12, 2019) kati ya FAO, Ujerumani na shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) wa kuzisaidia nchi zinazoendelea kushughulikia mabadiliko ya tabianchi katika sekta zao za kilimo.

FAO itaendelea kushirikiana na kwa karibu na wadau wote katika mfumo wa Umoja wa Mataifa, nchi, asasi za kiraia, sekta binafsi, wanazuoni na washirika wote muhimu ili kuongeza ufanisi wa suluhu zilizopo na kuhakikisha kwamba suluhu za asili zinasalia kuwa kitovu kwa hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na kulinda bayoanuai.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
16 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
16 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
16 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Magonjwa haya matano yanayoongoza kwa kuua watu duniani

Magonjwa haya matano yanayoongoza kwa kuua watu duniani

Nukta TV

Mambo yakuzingatia kabla ujawasha gari lako asubuhi

Mambo yakuzingatia kabla ujawasha gari lako asubuhi

Nukta TV

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Nukta TV