Kinachowasukuma vijana kubagua baadhi ya kazi

April 2, 2020 12:06 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Sababu ni pamoja na elimu wanayoipata, mkumbo wa kutaka kuwa kama rafiki zao na msukumo wa ndoto binafsi.
  • Lakini wametakiwa kubadilisha mtazamo na kujaribu kufanya kazi mbalimbali halali ili ziwatoe kimaisha.

Dar es Salaam. Kama wewe ni kijana mchapa kazi usiyechagua kazi, hakika unahitaji pongezi. Lakini unajisikiaje ukikutana na rafiki yako ambaye amekuwa akilalamika kuwa hawezi kufanya kazi fulani kwa sababu siyo ya hadhi yake?

Tabia hiyo huwakumba vijana wengi wahitimu wa vyuo vikuu ambao wamesomea taaluma mbalimbali. Malengo yao ni kupata kazi za ofisini (White job). 

Kutokana na uhaba wa nafasi za ajira Serikalini na sekta binafsi, hujikuta wakikaa nyumbani kwa muda mrefu na kuendelea kutuma maombi ya kazi bila mafanikio. 

Benki ya Dunia (WB) inakadiria vijana wapatao 800,000 huingia katika soko la ajira Tanzania kila mwaka lakini ni takriban asilimia 10 tu ndiyo hufanikiwa kupata kazi. 

Suala la ongezeko la vijana wasio na ajira ni jambo linaloumiza vichwa vya wengi wakiwemo viongozi wa Serikali na jamii kwa ujumla, licha ya sera na sheria mbalimbali kuainisha kupata kazi kama haki muhimu kwa vijana.

Lakini baadhi ya vijana hasa wale waliosoma wanaweza kuwa sababu ya kuzidisha tatizo hilo kwa sababu hawaoni umuhimu wa kuanzia chini kusaka fursa za kazi za kujiajiri au kuajiriwa.

Kutokana na uhaba wa nafasi za ajira Serikalini na sekta binafsi, hujikuta wakikaa nyumbani kwa muda mrefu na kuendelea kutuma maombi ya kazi bila mafanikio. Picha| Raw story.

Mkufunzi wa waajiriwa na waajiri, Moses Samora amesema “vijana wengi wamezaliwa kuona maisha yanasonga kwa hiyo hawajakuzwa kuona jinsi ya kuishi katika mchakato ili kujijenga.”

Hali hiyo imewafanya kutokuona umuhimu wa kuanzia chini ili waweze kupanda juu siku hadi siku.

Wakati meingine inaweza kumuumiza sana kijana kichwa baada ya kumaliza chuo na kuwaona baadhi ya marafiki zake wakipata kazi nzuri na kujipa matumaini kuwa na yeye anaweza kupata kazi kama za wenzake.

Lakini anasahau kuwa kila mtu ana njia yake ya kufanikiwa, muhimu ni kuanzia pale ulipo hata kama ni chini kiasi gani.

Meneja wa kiwanda cha kusaga unga cha Lina Millers ltd kilichopo Jijini Dar es Salaam, Christian Koyage amesema pia msukumo wa wazazi na ndoto kubwa walizonazo vijana vinaweza kuwafanya kuumia kichwa kiasi cha kupoteza mwelekeo na kukurupuka kwenye kufanya maamuzi.

Ni katika kipindi hicho ambapo hata fursa za ndogo ndogo ambazo zinaweza kumsaidia kupunguza makali ya kukosa ajira atazipuuzia.


Zinazohusiana


Lakini kama wewe ni miongoni mwa vijana hao, bado una nafasi ya kutoka katika mkwamo huo na kufanya mambo makubwa ikiwa tu utaacha tabia ya kuchagua kazi. 

Mwakilishi wa Tanzania kwenye Baraza la Biashara la Afrika Mashariki (EABC), Raphael Maganga amesema kijana aliyemaliza chuo hasa katika umri wa kati ya miaka 20 hadi 30  kijana yeyote hatakiwi kuchagua kazi kwa sababu ni kipindi cha majaribio na kupata ujuzi na maarifa.

Kwa kufanya hivyo, kijana yeyote atajengewa uwezo wa uvumilivu na nidhamu ya kazi kuliko kama akiingia kwenye mafanikio hayo moja kwa moja.

Naye Samora ambaye licha ya kuwa na Shahada ya Uzamili  alianzia chini  kama “trainee” wa meneja rasilimali watu amesema ipo haja ya kuwaonyesha na kuwaelimisha vijana kuwa hakuna kinachokuja kirahisi.

Na hilo linaweza kufanyika kwa kuanza kubadili mitazamo yao.

Je, wewe unafikiri vijana wanatakiwa kufanya nini ili asione aibu hata akiwa anauza sharubati mtaani? Tuandikie kwenye kurasa zetu za mitandao ya kijamii.  

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: LIVE:WABUNGE WAKIWACHAPA MASWALI MAWAZIRI | Bunge la 13 | Kikao cha 28

🔴LIVE: LIVE:WABUNGE WAKIWACHAPA MASWALI MAWAZIRI | Bunge la 13 | Kikao cha 28

Nukta TV

Top 10 ya magari yanayotumia kiwango kidogo cha mafuta

Top 10 ya magari yanayotumia kiwango kidogo cha mafuta

Nukta TV

SGR yaingizia Serikali Sh169.37 bilioni tangu kuanza kwa safari Juni 2024

SGR yaingizia Serikali Sh169.37 bilioni tangu kuanza kwa safari Juni 2024

Nukta TV