Ahueni: Serikali ikipendekeza ongezeko la kiwango cha mapato ya waajiriwa

June 11, 2020 2:43 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Imependekeza wafanyakazi wote wenye mapato ya jumla yasiyozidi Sh3,24 milioni kutokuwa na kiwango cha kodi.
  • Wafanyakazi wenye mapato ya jumla zaidi ya Sh12 milioni kutozwa asilimia 30 pamoja na kiasi zaidi ya Sh1.5 milioni.
  • Lengo la mabadiliko haya ni kutoa unafuu wa kodi ya mapato kwa wafanyakazi.

Dar es Salaam. Serikali inakusudia kufanya marekebisho katika Sheria ya Kodi ya Mapato sura 332 yatakayopandisha kiwango cha mapato ya waajiriwa ili kuongeza kiwango cha mapato yasiyotozwa kodi (threshold).

Waziri wa Fedha na Mipango Dk Philip Mpango amesema kwa mwaka ujao wa 2020/21 Serikali itaipandisha kiwango cha mapato ya waajiriwa kutoka Sh170,000 hadi Sh270,000 kwa mwezi.

Hiyo ni  sawa na kutoka Sh2.1 milioni hadi Sh3.3 milioni kwa mwaka.

“Lengo la mabadiliko haya ni kutoa unafuu wa kodi ya mapato kwa wafanyakazi. Hatua hii pekee inatarajiwa kupunguza mapato kwa Sh517.2 milioni,” amesema Dk Mpango.

Waziri huyo amependekeza kuwa, Mapato ya jumla yasiyozidi Sh3.24 milioni yasiwe na kodi huku mapato ya jumla yanayozidi Sh3.24 milioni lakini hayazidi Sh 6.24milioni kiwango cha kodi kiwe cha asilimia 9.


Zinazohusiana


Pia, kwa wafanyakazi wenye mapato ya jumla yanayozidi Sh6.24.miloni lakini hayazidi Sh9.12 milioni  mapendekezo ni tozo ya Sh270,000 pamoja na asilimia 20 kwa kiasi kinachozidi Sh6.24 milioni.

Kwa upande wa wafanyakazi wenye mapato ya jumla yanayozidi Sh9.12 milioni lakini hayazidi Sh12.0 milioni yatozwe kodi kwa kiwango cha Sh846,000 pamoja na asilimia 25 kwa kiasi kinachozidi Sh9.12 milioni.

Na kwa wafanyakazi wenye mapato ya jumla yanayozidi Shilingi 12.0 milioni yatozwe kodi ya Sh1.566 milioni pamoja na asilimia 30 ya kiasi kinachozidi Sh12,0 milioni.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV