“Da 5 Bloods”: Filamu itakayokufundisha maana halisi ya uzalendo

June 19, 2020 10:23 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni filamu inayohusu wapiganaji wa vita wanne waliompoteza rafiki yao kipindi cha vita ya Marekani na Vietnam.
  • Wanaanza safari ya kutafuta mabaki ya mwili wa rafiki yao baada ya miongo mingi kupita.
  • Siyo rafiki yao tu, na shehena ya dhahabu ambayo waliificha enzi za vita.

Dar es Salaam. Huwa unapata hisia gani pale unaposikia neno uzalendo? Usiniambie ni sualala kuipenda nchi yako kwa maneno. 

Mbali na maana yake uliyoisoma katika somo la uraia, utaongezea maana nyingine kupitia filamu hii ya “Da 5 Bloods” ambayo unaweza kuitaza katika mtandao wa Netflix. 

Wapiganaji wanne wa vita wanaungana kuanza safari ya kurudi katika uwanja wa mapambano miongo mingi baada ya vita waliyopigana baina ya Marekani na Vietnam.

Lengo kubwa ni kutafuta mabaki ya kiongozi wao wa vita, Chadwick Boseman (Black Panther) ambaye kwa mujibu wao ni “mwanajeshi bora kuwahi kukanyaga uso wa dunia.”

Wapiganaji hao Paul (Delroy Lindo), Otis (Clarke Peters), Eddie (Norm Lewis) na (Isiah Whitlock Jr) wanalazimika kukabiliana na vihunzi vya kimazingira na vya binadamu kutafuta mwili wa rafiki yao na shehena ya dhahabu ambazo Boseman aliwasihi kuzificha ili zinufaishe watu ambao watoto wao walikufa vitani.


Zinazohusiana


Andaa mbavu zako kufurahia visa huku tishu yako ikiwa tayari kufuta machozi pale mambo yanapoenda kombo katika filamu hiyo. 

Watazipata dhahabu hizo? Watayapata mabaki ya  mwili wa kiongozi na rafiki yao? Ni wewe wa kujibu hayo kwa kuitazama filamu hii kupitia mtandao wa Netflix endapo umelipia kifurushi chako.

Wiki ijayo kuna nini?usicheze mbali na ukurasa huu. 

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Nukta TV

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Nukta TV

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Nukta TV