Huu ndiyo uchungu wa mwana kwa mzazi wake

September 11, 2020 1:10 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni filamu inayomhusu mwanadada Enola ambaye amelelewa na mama yake pasi kujua mafunzo ya kuwa binti katika jamii yake.
  • Wakati mabinti wenzake wanatengeneza mavazi, Enola ni mwana sayansi na mpiganaji.
  • Hata hivyo, uchungu wa mwana kwa mzazi unaingia pichani baada ya mama yake kupotelea kusikojulikana.

Dar es Salaam. Tuanzie wapi? Enola amezaliwa na mama yake! Hahaha, kusimulia hadithi inaweza kuwa changamoto.

Tofauti na wasichana wengine ambao baada ya kuzaliwa hufundishwa kazi ambazo jamii imezitenga maalumu kwa wanawake yaani kupika na kufanya usafi na zinazohusiana na hizo.

Lakini Enola alifundishwa kupigana, michezo na hata kuchangamana na kemikali yaani kuwa mwanasayansi na mengine yote wanayoyafanya wanaume. 

Ajabu ni kuwa aliyemfundisha mambo hayo ni mama yake.

Wakati amemzoea mama yake kiasi cha kutokutaka lolote la duniani liwatenganishe, Enola anajikuta hamuoni mama yake. Yaani anaamka na na anamtafuta nyumba nzima na hayupo.


Soma zaidi


Safari ya kumtafuta mzazi wake inaanza kwa kutaka kuungana na kaka zake ambao huenda jina la mmoja wao linaweza kugonga kengere masikioni mwako.

Sherlock Holmes. Ndiyo! Askari mpelelezi anayesifika dunia nzima kwa uwezo wake wa kunusa tukio la uhalifu na kulitatua hata pale dunia nzima inaposhindwa. 

Sherlock ambaye anaambatana na Mycroft Holmes hawana ujanja bali kumpokea Enola Holmes ambaye ni binti asiyejua jinsi ya kuwa binti kwenye jamii ya Waingereza.

Je, watafanikiwa kumpata mama yake na Enola? Fuatilia filamu ya Enola Holmes kwa mikasa na vitimbwi vya kuvunja mbavu kupitia mtandao wa Netflix ifikapo Septemba23 2020.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
19 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
19 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Siku ya Familia, Mtoto wa Afrika kuadhimishwa Juni 30, 2026

Siku ya Familia, Mtoto wa Afrika kuadhimishwa Juni 30, 2026

Nukta TV

Wadau wa 'kubet" watoa ya moyoni, pendekezo kupanda kwa tozo 5%

Wadau wa 'kubet" watoa ya moyoni, pendekezo kupanda kwa tozo 5%

Nukta TV

Wasemayo wananchi, vocha za kukwangua kupigwa maruku mijini

Wasemayo wananchi, vocha za kukwangua kupigwa maruku mijini

Nukta TV