Ahueni, maumivu: Bei ya mchele Katavi, Dar

September 28, 2020 11:34 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Bei ya jumla ya zao hilo katika jiji la Dar es Salaam ni zaidi ya mara tatu ya inayotumika Mpanda ambayo ni Sh70,000. 
  • Wafanyabiashara wa jijini humo kulala na tabasamu. 

Dar es Salaam. Wafanyabiashara wa mchele katika jiji la Dar es Salaam leo watalala na tabasamu baada ya bei ya jumla inayotumika kuuza za hilo ni zaidi ya mara tatu ya ile ya Mkoa wa Katavi.

Mchele ni miongoni mwa mazao makuu ya chakula yanayotegemewa na Watanzania kwa ajili ya matumizi mbalimbali ikiwemo chakula. Mazao mengine ni mahindi, mtama, maharage, viazi mviringo na mihogo. 

Takwimu za mazao makuu ya chakula zilizotolewa na Wizara ya Viwanda na Biashara leo (Septemba 28, 2020) zinaonyesha kuwa gunia la kilo 100 la mchele linauzwa kwa Sh230,000 katika soko la Tandika jijini Dar es Salaam.  

Bei hiyo ya jumla ni zaidi ya mara tatu ya ile ya Sh70,000 inayotumika katika Wilaya ya Mpanda katika Mkoa wa Katavi, jambo linalofaidisha zaidi wafanyabiashara na wakulima wanaouza zao hilo katika jiji hilo. 

Bei inayotumika jijini humo, ndiyo bei ya juu ikilinganishwa na mikoa mingine huku inayotumika Mpanda ndiyo bei ya chini kabisa. 

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
26 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
26 May, 2026
No active movers today
Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

Nukta TV

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

Nukta TV

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

Nukta TV