Alama muhimu zitakazokuwezesha kutambua noti halali ya Sh10,000

September 30, 2020 6:12 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Noti hiyo ina alama 11 za usalama ikiwemo ya mnyama Twiga na Sura ya Hayati Mwalimu Julius Nyerere. 
  • Imewekewa alama kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa kutokuona. 
  • Alama hizo zitakusaidia kufahamu noti unayotumia kama ni halali au ya kughushi. 

Dar es Salaam. Huenda wewe ni miongoni mwa watu ambao wanashindwa kutofautisha noti halali na bandia (iliyogushiwa) ya Tanzania hasa ya Sh10,000, usihofu maana suluhu imepatikana. 

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa ufanunuzi wa alama 11 muhimu zinazopatikana katika noti ya Sh10,000 ambazo zitakusaidia kufahamu kama noti unayotumia ni halali au imegushiwa ili kukuepusha na mkono wa sheria. 

Ikumbukwe kuwa kughushi noti halali za fedha ya Tanzania ni kosa kisheria kwa mujibu wa Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya mwaka 2006.

Alama 11 zinazopatikana katika noti ya Sh10,000 ambazo zitakusaidia kutambua kama noti unayotumia ni halali. Picha| Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Alama hizi 11 zinazopatikana pande zote mbili za noti ya Sh10,000 zitakusaidia kufahamu kwa usahihi noti halali kwa kuiona kwa macho au kutumia mwanga:

1.Sura ya Mwalimu Julius Nyerere

BoT inaeleza kuwa uwepo wa alama iliyofichika kwenye noti inayoonesha sura ya Rais wa kwanza wa Tanzania, Hayati Mwalimu Julius Nyerere na thamani ya noti ya Sh10,000, utakusaidia kufahamu kuwa noti hiyo ni halali. 

2.Vipande vya thamani ya Sh10,000

Katika noti hiyo utakutana na alama za vipande vipande zenye kuonyesha thamani ya noti ya Sh10,000 na inapomulikwa kwenye mwanga tarakimu kamili za thamani ya noti hutokea. 

Kama zisipotokea kwenye mwanga, basi fahamu noti hiyo siyo halali kwa matumizi.

Alama hizo mbili za Sura ya Hayati Mwalimu Julius Nyerere na vipande vya thamani ya Sh10,000 ni mbinu ya kubaini noto halali. Picha| Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

3. Kivuli kilichofichika

Alama maalum iliyofichika yenye kuonyesha thamani ya noti ya Sh10,000 huonekana kuwa angavu noti inapogeuzwa geuzwa. 

4. Alama maalum kwa walemavu wa macho

Kwa mujibu wa BoT, noti halali ya Sh10,000 inaweza kutambuliwa na hata watu wenye ulemavu wa kutokuona. Kuna alama za pembe zinazoparuza na alama maalum zinazotambulisha thamani ya noti kwa kuipapasa kwa wenye ulemavu wa macho. 

Alama hizo namba 3 na 4 nazo zitakusaidia kuifahamu kwa undani noti ya Sh10,000. Picha|Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

5. Alama maalum ya Twiga

Alama maalum ambayo Twiga anaonekana ndani yake, yenye rangi ya dhahabu ambayo hubadilika kuwa kijani na kurudia tena kuwa ya dhahabu pale noti inapogeuzwa.

 

6. Uwepo wa maandishi madogo yaliyolala

BoT inaeleza kuwa katika noti hiyo pia yanapatikana maandishi madogo sana yaliyolala na kutuna yanayoonekana kwa kutumia vifaa maalum vya kukuzia maandishi. 

Alama ya mnyama Twiga nayo itakusaidia kuithibitisha noti ya Sh10,000. Picha| Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

7. Nyuzi nyembamba zenye rangi tatu

Nyuzi nyembamba zenye rangi tatu zilizofichika ambazo huonekana kwa kutumia mwanga maalum wa rangi ya zambarau. Nyuzi hizo zitakusaidia kufahamu kuwa noti uliyoshika mkononi ni halali.

8. Alama ya kubadilika kwa rangi kwenye utepe mwembamba

Alama hiyo ya ya usalama iliyoboreshwa kwenye utepe mwembamba upande wa juu kushuka chini inaonyesha kutembea na kubadilika kwa rangi. 

Rangi za utepe huo zinaonyesha upinde wa mistari mithili ya mawimbi yanayotembea kutoka kushoto kwenda kulia na kinyume chake.

“Pale noti hiyo inapogeuzwa geuzwa upande wa juu na chini, rangi za utepe huo zinabadilika toka rangi ya pinki kwenda kijani. Pia, unapoielekeza kwenye mwanga, kuna maneno yanayosomeka ‘BOT 10000’,” inaeleza BoT.

9. Alama ya wino maalum 

Alama hiyo ya wino uliofichika huangaza noti ikimulikwa kwa mwanga wa rangi ya zambarau. Alama hiyo ipo katikati ya majengo pacha ya BoT yaliyopo kwenye noti hiyo. 

Uwepo wa alama hizi tatu katika noti ya Sh10,000 zinaifanya noti hiyo kuwa halali kwa matumizi. Picha| Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

10. Namba ya noti 

Namba hiyo ya noti yenye tarakimu zinaongezeka ukubwa na kung’aa zinapomulikwa kwa mwanga maalum wa rangi ya zambarau.

11. Alama ya wino maalum 

Alama hiyo iliyofichika ambao huonekana noti ikimulikwa kwa mwanga maalum wa rangi ya zambarau. 

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Unaweza kusema ni maumivu juu ya maumivu kwa watumiaji wa vyombo vya moto vinavyotumia mafuta ya

Unaweza kusema ni maumivu juu ya maumivu kwa watumiaji wa vyombo vya moto vinavyotumia mafuta ya

Nukta TV

Neema Mohamed, Mkurugenzi wa Bone and Blood Foundation, ni shujaa wa ugonjwa wa selimundu Sickl

Neema Mohamed, Mkurugenzi wa Bone and Blood Foundation, ni shujaa wa ugonjwa wa selimundu Sickl

Nukta TV

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ametua kwenye ardhi ya Urusi kwa ziara ya kitaifa ya siku

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ametua kwenye ardhi ya Urusi kwa ziara ya kitaifa ya siku

Nukta TV