Siri iliyofichika watoto mapacha kuhusishwa na “mikosi” Kanda ya Ziwa–3

November 20, 2020 8:15 am · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Mkango hutakiwa kufanya tambiko kila anapozaa mapacha.
  • Gharama za tambiko ikiwemo chakula, zawadi kwa mtemi vyote huwa juu ya anayefanyiwa tambiko.
  • Baadhi ya watu hushindwa kumudu gharama hizo kwa sababu ya umaskini. 

Mwanza. Katika mfululizo wa makala haya, sehemu hii inaangazia gharama za kufanikisha matambiko ya “kuondoa laana kwa mapacha na jinsi ambavyo watu wanashindwa kutimiza masharti ya mila hiyo”. 

Gharama ya kufanya tambiko la Wakango ni zaidi ya kuwa na pesa, linahusisha masharti mengi ambayo mhusika anapaswa kutimiza bila kuacha moja kulingana na aina ya mapacha aliozaa. 

Wakango wananijuza kuwa endapo mama akifanikiwa kujifungua mapacha zaidi ya mara moja, siyo kwamba atafanya tambiko mara moja pekee, isipokuwa kila uzao wa mapacha atakaojaaliwa na mwenyezi Mungu lazima uufanyie tambiko.

“Nilibahatika kuzaa mapacha mara nne, akina Kulwa na Dotto mara mbili na Akina Kashinje mara mbili, na wote kwa nafasi yake niliwafanyia tambiko,” anasema Mindi Shigella ambaye yuko kwenye sherehe hizo kuwapokea Wakango wapya akiwemo Mzee Shibiriti.

Anasema kanuni na taratibu hizo ziliwekwa toka matambiko haya yaanze kwani kila mmoja huja na mikosi yake hivyo ukiamua kufanya tambiko moja ukiamini kuwa umemaliza hapo utakuwa umejidaganya.

Wakati wa kufanyiwa tambiko kuna dawa zinawekwa kwa ajili ya kuwalinda mapacha na ikitokea mmoja kati ya hao akatangulia mbele za haki basi watemi kwa kushirikiana na waganga huwa wanamtengenezea pacha mwenzie.

Pacha huyo anayekuwa kwenye mfano wa hirizi anayovikwa shingoni anavalishwa pacha aliyesalia na atakuwa anatembea nayo popote atakapoenda.

Pacha (hirizi) huyo wa kutengenezwa ambaye wakati mwingine huwa ni kibuyu kidogo huvaliwa  shingoni au kufungwa sehemu yoyote ya mwili baada ya wazee wa mila kuipitisha. 

“Ukitaka kuondoka utambusu na ukitaka kufanya jambo utamshirikisha na kwa imani kabisa tunaamini kuwa huwa anasikia, kwa mfano mimi sijaja naye hapa lakini kabla sijaondoka nyumbani nilimuaga nikamuomba asijisikie vibaya na nitarudi na nitamkuta salama,” anasema Mzee Kulwa Mabirika ambaye mwenzake Dotto alifariki dunia. 

Mzee huyo anasema huwa wanafanya hivyo ili kuondoa upweke kwa yule anayebaki.

Moja ya tambiko la kupitishiwa vyungu vitatu vilivyo na ugali, kitoweo na mboga jamii ya kunde ambapo wazazi wa watoto mapacha hutakiwa kula kijeshi wakati vyungu hivyo vikipitishwa mbele na nyuma. Picha|Mariam John.


Mfuko nao hutoboka kweli kweli

Licha ya kuwa sherehe za matambiko huwa ni furaha lakini huacha maumivu kwa mtu anayefanyiwa tambiko kwa sababu hutakiwa kubeba gharama zote zinazohitajika kukamilisha taratibu hizo.

Mathalan, katika shughuli za tambiko nilizohudhuria kwa siku tatu mfululizo katika kijiji cha Mwamajila, Mzee Shibiriti na familia yake wametumia zaidi ya Sh3 milioni kwa ajili ya shughuli hiyo.

Fedha hizo zinatumika kununua chakula cha wageni, zawadi kwa Mtemi  wa Wakango, malipo kwa Manju (mwimbishaji nyimbo) na wapiga ngoma wake sambamba na malipo ya Nsumba Ntale.

Mtemi Emmanuel Mkwaga anasema kabla ya kukubali kufanyiwa tambiko la kuondoa mikosi, wahusika hutakiwa kuridhia kwanza kujiunga na Wakango na wanatakiwa (mke na mume) kila mmoja kutoa gunia moja na debe mbili za karanga, kondoo au mbuzi watano kila mmoja, na kiasi cha Sh60,000.

“Vitu hivi hutolewa ili vitumike kwa ajili ya chakula cha Wakango wakati wa matambiko, huku karanga na hela hugawana Wakango,”anasema Mtemi Mkwaga.


Soma zaidi:


Kwa mujibu wa maelezo ya mtemi huyo, endapo mmoja wapo akashindwa kukamilisha vitu hivyo matambiko hayataweza kufanyika.

Gharama hizo huwakatisha tamaa baadhi ya watu wanaozaa mapacha na hivyo kushindwa kutimiza mila hizo.

Siyo fedha tu ambazo anayefanyiwa tambiko anatakiwa kulipa, bali kushiriki kikamilifu mchakato wa tambiko ambao unafanyika kwa siku tatu mfululizo. 

Wakati Wakango wakiamini mapacha ni mikosi na wanatakiwa kufanyiwa tambiko, watu wengine wamekuwa na maoni tofauti kuhusu mila hiyo. Sehemu inayofuata itajadili kwa undani mitazamo hiyo.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Unaweza kusema ni maumivu juu ya maumivu kwa watumiaji wa vyombo vya moto vinavyotumia mafuta ya

Unaweza kusema ni maumivu juu ya maumivu kwa watumiaji wa vyombo vya moto vinavyotumia mafuta ya

Nukta TV

Neema Mohamed, Mkurugenzi wa Bone and Blood Foundation, ni shujaa wa ugonjwa wa selimundu Sickl

Neema Mohamed, Mkurugenzi wa Bone and Blood Foundation, ni shujaa wa ugonjwa wa selimundu Sickl

Nukta TV

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ametua kwenye ardhi ya Urusi kwa ziara ya kitaifa ya siku

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ametua kwenye ardhi ya Urusi kwa ziara ya kitaifa ya siku

Nukta TV