Corona: Facebook yabana zaidi wapotoshaji mtandaoni

March 5, 2021 8:47 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Baadhi ya maneno kama covid-19 imetengenezwa na watu au kuwa chanjo ni hatari na inaweza kusababishia ugonjwa wa usonji hayatonekana.
  • Pia sera hiyo itagusa akaunti  au makundi ya kwenye Facebook na Instagram ambayo yamekuwa yakirudi kuchapisha taarifa ambazo tayari zimesha thibitishwa kuwa ni za uzushi lakini wao bado wanarudia kuzichapisha.

Dar es Salaam. Kampuni ya Facebook Inc imeongeza wigo wa kupambana na habari za uzushi zinazohusu janga la Corona na chanjo kwa kutoa orodha ya maneno ambayo yatatiliwa mkazo katika vita yake dhidi ya habari hizo mtandaoni. 

Huo ni muendelezo wa kampuni hiyo kuwalinda watumiaji wake dhidi ya uzushi unaosambazwa na watu wenye nia mbaya. 

Katika taarifa iliyotolewa mwezi Februari 2021, Facebook imeeleza kuwa baada ya kushauriana na Shirika la Afya duniani (WHO), kampuni hiyo  imeamua kutanua wigo wake wa kupambana na habari za uzushi ulimwenguni kwa kutoa orodha ya maeneo ambayo yatatiliwa mkazo zaidi kwa watumiaji wa Facebook na Instagram. 

Maneno ambayo yametajwa katika orodha hiyo ni pamoja na taarifa kuwa Covid-19 imetengezwa na watu, ni bora kupata ugonjwa  wenyewe kuliko chanjo, chanjo ni hatari na inaweza kusababisha ugonjwa wa usonji.


Zinazohusiana:


Kutolewa kwa orodha hiyo ni mwendelezo wa  sera ya Facebook inayosimamia habari na taarifa zinazochapishwa katika mitandao yake ya kijamii. 

“Sera hizi mpya zitatusaidia kuendelea kuchukua hatua kali dhidi ya taarifa za uongo kuhusu COVID-19 na chanjo,” imeeleza sehemu taatifa ya Facebook. 

Rungu hilo litawazifikia habari za uzushi zinawekwa kwenye kurasa za mtandao huo na makundi ya Facebook na Instagram.

Facebook imesisitiza kuwa itaendelea kuchukua hatua kali dhidi ya taarifa zote zinazokinzana na sera zake za maudhui ambapo zitawekewa alama  na kuondolewa kabisa kwenye mitandao yake. 

Kwa hatua hizo, ilizochukua Facebook, unafikiri utakuwa salama dhidi ya habari za uzushi kuhusu COVID-19?

Enable Notifications OK No thanks