Mikoa nane kunufaika na vifaa vya kutokomeza TB Tanzania

August 6, 2021 3:05 pm · TULINAGWE ALSON
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni vifaa vitakavyosaidia kukusanya sampuli ili zipimwe kwa wakati katika vituo vya afya na kubaini wagonjwa. 
  • Ni sehemu ya mradi unaolenga kutambua asilimia 41 ambayo inaishi na kifua kikuu bila kugundulika.
  • Mradi huo utahusisha mikoa nane Bara na visiwani Zanzibar.

Dar es Salaam. Mikoa nane Tanzania inatarajiwa kunufaika na vifaa vitakavyosaidia kubaini zaidi ya theluthi ya watu wanaougua kifua kikuu nchini bila kujulikana ikiwa ni moja ya jitihada za kukabiliana na maradhi hayo. 

Vifaa hivyo ambavyo ni baiskeli 710 na vibebea sampuli 859 vimetolewa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID) kwa Serikali ili kupunguza maambukizi ya kifua kikuu nchini hasa kipindi hiki ambacho dunia imejikita zaidi katika kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona (Uviko-19).

Utoaji wa vifaa hivyo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi unaolenga kutambua asilimia 41 ya watu wanaoishi na kifua kikuu bila kugundulika.

Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – Tamisemi Dk Grace Magembe amesema pamoja na kupunguza maambukizi itakua fursa muhimu kwa vijana wa bodaboda kujipatia kipato na kuimarisha afya zao kwa ujumla.

Katika kukabiliana na maradhi hayo,  vijana wa bodaboda 114 wanatarajiwa kuajiriwa ili kuwafikia waathirika ambao hawajagundulika na kupata matibabu katika mikoa ya Dar es Salaam, Geita, Mwanza, Kigoma, Pwani, Rukwa, Songwe, Katavi na visiwani Zanzibar. 

Katika mradi huo vijana wenye uzoefu wa kuendesha bodaboda kuziendesha baiskeli ili kuwafikia waathirika hao na kuchukua sampuli kutoka kwenye jamii kwenda kwenye vituo vya afya. 

Maofisa afya katika jamii watakuwa na kazi ya kukusanya sampuli hizo kwa ajili ya kwenda kupimwa kwenye vituo vya afya ili kubaini wagonjwa na kuwaanzishia tiba mapema na kuwaepusha na vifo. 

“ Hawa bodaboda wakipata ajira wataenda kujenga vijumba vyao vyenye mandhari nzuri na kuboresha maisha ya familia zao,” amesema Dk Magembe.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la afya Duniani (WHO) maambukizi  mapya ya ugonjwa wa kifua Kikuu nchini Tanzania yalipungua kwa asilimia 18 mwaka 2020 huku ikiendelea kuwa ni miongoni mwa nchi 30 zilizo na maambukizi mengi ya TB.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Nukta TV

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

Nukta TV

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Nukta TV