Mfumuko wa bei za bidhaa, huduma wapaa mfululizo kwa miezi sita

October 11, 2022 4:00 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Umefikia asilimia 4.8 mwaka unaoishia Septemba 2022.
  • Umekuwa ukipanda mfululizo tangu Aprili.
  • Kupanda kwa bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula kwachangia. 

Dar es Salaam. Mfumuko wa bei za bidhaa na huduma nchini umeendelea kupanda mfululizo kwa miezi sita hadi kufikia asilimia 4.8 kwa mwaka unaoishia Septemba 2022, ukichagizwa na kupanda kwa bei za bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula. 

Mfumuko wa bei wa Taifa hupima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi nchini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Oktoba 10, 2022 na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), mfumuko wa bei umepanda kutoka asilimia 4.6 iliyorekodiwa mwaka unaoishia Agosti 2022. 

“Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba, 2022 imeongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2022,” imeeleza NBS katika taarifa yake.  

Tangu Aprili mwaka huu mfumuko wa bei umekuwa ukipanda mfululizo ambapo mwaka unaoishia Machi 2022 ulikuwa asilimia 3.6 lakini baada ya hapo ukawa unapanda kwa viwango tofauti hadi ulipofika asilimia 4.8 mwaka unaoishia Septemba 2022.

Hata hivyo, NBS imesema mwenendo huo wa mfumuko wa bei ni imara. 

Baadhi ya bidhaa za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa mfumuko wa bei ni pamoja na mchele kwa asilimia 0.3, mahindi (asilimia 4.5), unga wa ngano (asilimia 0.2), unga wa mahindi (asilimia 3.2) na samaki wa maji baridi kwa asilimia 1.2.

Dagaa wakavu kwa asilimia 2.0, nazi (asilimia 3.0), karanga mbichi (asilimia 1.3), maharage makavu ya kawaida (asilimia 4.2) na maharage makavu jamii ya kombati kwa asilimia 4.9. 


Soma zaidi:


Baadhi ya bidhaa zisizo za chakula zilizochangia kuongezeka kwa mfumuko wa bei ni pamoja na vitambaa vya nguo kwa asilimia 0.6, nguo za wanaume (asilimia 0.5), viatu vya wanaume (asilimia 0.2), bidhaa kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa nyumba (asilimia 1.4) na gesi ya kupikia kwa asilimia 0.4.

Mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba, 2022 umeongezeka hadi asilimia 8.3 kutoka asilimia 7.8 kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2022. 

“Kwa upande mwingine, mfumuko wa bei ambao haujumuishi bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Septemba, 2022 umeongezeka hadi asilimia 3.5 kutoka asilimia 3.4 ilivyokuwa mwezi Agosti, 2022,” imeeleza NBS.  

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
25 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
25 May, 2026
No active movers today
Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

Nukta TV

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

Nukta TV

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

Nukta TV