Bei mpya za petroli, dizeli Novemba hizi hapa

November 1, 2022 3:53 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Bei ya dizeli yashuka.
  • Bei petroli itakua Sh2,886 iliyotumika Oktoba mwaka huu.

Dar es Salaam. Wamiliki wa vyombo vya moto kuanzia kesho wataanza kutumia bei mpya za mafuta baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) kutangaza bei kikomo huku baadhi zikishuka. 

Kwa mujibu wa Ewura katika taarifa yake kuhusu bei mpya zitakazoanza kutumika Novemba 2, 20222, bei ya mafuta ya rejareja ya dizeli kwa Dar es Salaam na Tanga imepungua kwa Sh31 kwa lita na Sh34 kwa lita, ikilinganishwa na bei hizo kwa Oktoba 2022  baada ya Serikali kutoa ruzuku. 

Dizeli inayopitia bandari ya Dar es Salaam inauzwa kwa Sh3,052 kwa lita kutoka Sh3,083 ya Oktoba huku ile inayoingilia bandari ya Tanga ni Sh3,074 kutoka Sh3,108. 

“Bei ya rejareja ya mafuta ya petroli kwa Bandari ya Dar es Salaam ingeongezeka kwa Sh110 kwa lita, hata hivyo, Serikali imetoa ruzuku ili bei iliyopo ya Oktoba 2022 isibadilike,” imesema Ewura.

Hiyo ina maana kuwa bei petroli itakua Sh2,886 iliyotumika Oktoba mwaka huu.

“Kwa upande wa Mtwara, hakuna meli ambayo imehusishwa kwenye bei kwa Novemba 2022 kwa sababu meli inategemewa kushusha mafuta mwishoni mwa Novemba 2022 na mafuta yake yatatumika Desemba 2022,” imeeleza taarifa ya Ewura. 

“Hivyo, abadiliko ya bei kwa Novemba 2022 kwa Mtwara ni kwa ajili ya kuhusisha taarifa sahihi ya meli husika iliyotumika kwenye bei za Oktoba 2022. 

Bei ya mafuta ya taa na bei ya petroli kwa Tanga imepungua kwa Sh164 kwa lita na Sh118 kwa lita ukilinganisha na bei zilizopita kwa sababu ya wastani wa bei ndogo zaidi ya mafuta yaliyosafishwa katika soko la dunia na gharama za usafirisha kwa bandari ya Tanga.

/
No matches found for this filter
30 May, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
30 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
30 May, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

Nukta TV

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

Nukta TV

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

Nukta TV