Wanasayansi wakataa madai mafuta ya mbegu za mimea kuhatarisha afya ya binadamu

November 3, 2022 9:15 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Wasema madai hayo hayana ushaidi wa kisayansi.
  • Wakubaliana kuwa baadhi ya vyakula vinavyopikiwa na mafuta hayo vinaweza kuhatarisha afya. 
  • Washauri watu waendelee kutumia. 

Dar es Salaam. Wakati intaneti ikiwa na taarifa nyingi zinazoelezea kuwa mafuta ya mbegu za mimea yakiwemo kanola kuwa ni ‘sumu mwilini’, tafiti za kisayansi hazikubaliana na madai hayo. 

Mafuta ya kula yanayotokana na mbegu za mazao mbalimbali yamekuwa yakitumiwa katika shughuli mbalimbali ikiwemo kupikia chakula majumbani.

Hata hivyo, baadhi ya watu wakiwemo watalaam wa lishe wamekuwa wakidai kuwa mafuta hayo siyo salama kwa afya ya binadamu kwa sababu huchangia mtu kupata lehemu mbaya mwilini ambayo inaweza kuchangia mtu kupata magonjwa mbalimbali ikiwemo ya moyo. 

Kwa mujibu wa mtaalam Guy Crosby, mshirika msaidizi  wa lishe katika Shule Kuu ya Afya ya Umma ya Chuo Kikuu cha Harvard  cha nchini Marekani  amesema madai hayo hayana ushaidi wa kisayansi na hakuna madhara ya moja kwa moja kwa binadamu.

Crosby alinukuliwa Mei 31, 2022 katika andiko la Ripoti za Walaji akisema madhara yanayotajwa hayachangiwi moja kwa moja na mafuta hayo, hivyo anaamini siyo sahihi kuwakataza watu kutumia bidhaa hizo kwa shughuli za kupikia. 

Hata hivyo, ni ukweli usiopingika kuwa vyakula vingi vinatengenezwa kwa mafuta ya kula ya mbegu kama vitafunwa na chips siyo rafiki kwa afya kwa sababu vina kiasi kikubwa cha wanga, madini ya sodium na sukari. 

“Ni kweli ukipunguza matumizi ya vyakula hivyo,  una nafasi kubwa ya kuwa na afya njema,” alisema Crosby. 

Mtaalam huyo wa lishe amesema ikiwa mafuta hayo yatachomwa kwa moto mkali na kutumiwa bila kubadilishwa hasa wakati wa kukaanga vyakula kama inavyofanyika kwenye migahawa, kunaweza kuwa na athari za kiafya

Hata hivyo, amesisitiza kuwa, “kupikia mafuta ya mbegu nyumbani siyo tatizo.”

Wataalam wanaeleza zaidi kuwa hakuna haja ya kuachana na vyakula vyenye Omega 6, aina ya mafuta inayopatikana kwenye mafuta ya mbegu ikiwemo karanga na korosho.  Hiyo ni kwa sababu mlo wenye vyakula hivyo unasaidia kushusha lehemu, sukari kwenye damu na hatari ya kupata magonjwa ya moyo.

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Nukta TV

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Nukta TV

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Nukta TV