Simulizi ya wajawazito zaidi ya 350,000 walionusurika kifo tetemeko la Uturuki, Syria

February 20, 2023 12:08 pm · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Wanusurika kifo katika matetemeko yaliyoua zaidi ya watu zaidi ya 46,000.
  • Wanahitaji msaada wa huduma za afya ili wajifungue salama. 

Dar es Salaam. Familia na ndugu zao walikuwa wana matumaini lukuki kuwa siku au miezi michache ijayo watakuwa na furaha isiyo na kifani. Ni kuongeza idadi ya watu katika familia zao. 

Hata hivyo, matumaini hayo yalitaka kukatishwa na matetemeko ya hivi karibuni katika nchi za Uturuki na Syria yaliyoweka rehani maisha ya watu wa nchi hizo wakiwemo wanawake wajawazito. 

Licha ya kuwa matetemeko hayo yaliua watu zaidi ya 46,000, baadhi ya watu  wana kila sababu ya kushukuru kwa sababu uhai haujaguswa na janga hilo.

Miongoni mwa walionusurika katika matetemeko ya ardhi, ni wajawazito 356,000 ambao wanahitaji kupata huduma za afya ya uzazi kwa dharura.

Kati ya wajawazito hao, 226,000 kutoka nchini Türkiye na 130,000 nchini Syria, na kati yao takriban 38,800 wanatarajiwa kujifungua Machi mwaka huu.

Wakiwa wamepoteza wapendwa wao, nyumba zao na mali zao zote, wengi wa wajawazito hao wanajihifadhi katika kambi za muda au wanaishi katika mazingira ya baridi kali, na kujitahidi kupata chakula au maji safi, na hivyo kuhatarisha afya zao.

Maelfu ya majengo, ikiwa ni pamoja na hospitali na vituo vinavyoungwa mkono na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Idadi ya Watu (UNFPA) katika nchi hizo yameporomoka au kuharibiwa, na hivyo kukata kabisa fursa ya wanawake kupata taarifa na huduma za afya ya uzazi na kujamiiana pale wanapozihitaji.

“Katikati ya uharibifu uliozikumba nchi hizi za Syria na Türkiye, wanawake na wasichana walioathiriwa na matetemeko ya ardhi lazima wawe salama na walindwe, na waweze kupata huduma bora za afya ya ngono na uzazi wakati wanapohitaji,” amesema Mkurugenzi Mtendaji wa UNFPA Dk Natalia Kanem. 

Dk Kanem ametaka huduma hizo pia zijumuishwe kama sehemu muhimu ya misaada kwa mataifa hayo.

Watoto wanne walizaliwa kwa njia ya upasuaji katika Hospitali ya Al Fardous inayoungwa mkono na UNFPA katika Jiji la Daret Azza, katika wilaya inayoshikiliwa na waasi ya Jebel Saman katika Mkoa wa Aleppo, muda mfupi baada ya tetemeko la ardhi lililoharibu Uturuki na Syria. Picha | UN News.

Mwitikio wa kibinadamu wa UNFPA unalenga katika kutoa taarifa na huduma za afya ya uzazi zinazookoa maisha kwa wanawake na wasichana wanaohitaji, popote walipo.

Misaada ya kibinadamu inayotolewa na UNFPA unalenga katika kutoa taarifa na huduma za afya ya uzazi. Shirika hilo pia linatoa taarifa za kujilinda na huduma kwa wanawake na wasichana wenye uhitaji wowote walipo.


Hatua zinazochukuliwa

Nchini Türkiye, UNFPA inafanya kazi na wadau wake huko Diyarbakir, Sanliurfa, Adana, Mersin, Adiyaman na Hatay, ambapo wanatoa taarifa na huduma za afya ya uzazi na ulinzi kupitia timu za watu wanaozunguka sehemu moja hadi nyingine ambao wanatoa huduma katika maeneo yaliyoathirika.

“Wadau wetu wanapeleka timu zinazozunguka kwenye miji iliyoathirika na kutoa elimu ya afya ya ngono na uzazi na pia wanazungumza kuhusu unyanyasaji wa kijinsia,” amesema Dk Kanem.


Soma zaidi:


Timu hizo pia zinatoa huduma kwa wajawazito, baada ya kujifungua, na watoto wachanga, timu hizi huelekeza walengwa mahali kwenye huduma za uzazi na dharura za uzazi, na kutoa usaidizi wa kisaikolojia kwa waathirika wa kijinsia baada ya tetemeko la ardhi. 

Pia wanatoa vifaa vya kujistiri na vifaa vya msingi vya usafi na vifaa vya uzazi na vitu vingine muhimu kwa akina mama waliotoka kujifungua pamoja na watoto wao.

Nchini Syria, UNFPA inafanya kazi na wadau wake kusaidia vituo vya afya kutoa huduma muhimu za afya ya uzazi, ikiwa ni pamoja na usaidizi wa kisaikolojia na kijamii, na kuimarisha shughuli za mawasiliano na zahanati zinazohamishika katika jamii zilizoathirika zaidi.

Ndani ya saa 72 za matetemeko ya ardhi, UNFPA ilisafirisha dawa na vifaa vya kuokoa maisha vya afya ya uzazi kuvuka mpaka hadi kaskazini-magharibi mwa Syria ili kukidhi mahitaji ya watu 150,000 katika maeneo ya Serikali na yasiyo ya Serikali.

Huduma ya simu ya dharura pia imeanzishwa kusaidia wanawake wanaokabiliwa na ukatili na unyanyasaji huku maeneo salama 20 huko Aleppo, Hama na Latakia yakiendelea kutoa huduma za kuzuia na kukabiliana na unyanyasaji wa kijinsia.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
25 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
25 May, 2026
No active movers today
Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

Nukta TV

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

Nukta TV

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

Nukta TV