Kicheko, maumivu bei ya mahindi ikipanda

April 21, 2023 6:54 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Imepanda kwa asilimia 84.1  ndani ya kipindi cha mwaka mmoja unaoishia Februari 2023.

Dar es Salaam. Huenda Watanzania wakaendelea kutoboa mifuko yao zaidi baada ya bei ya mahindi kupanda kwa asilimia 84.1  ndani ya kipindi cha mwaka mmoja unaoishia Februari 2023.

Mahindi ni sehemu ya mazao makuu ya chakula yanayotumiwa kwa wingi na Watanzania. Mazao mengine ni maharage, mtama, uwele na viazi.

Ripoti ya Tathmini ya Uchumi ya Machi 2023 (Monthly Economic Review) iliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) hivi karibuni imeeleza kuwa bei ya jumla ya gunia la kilo 100 la mahindi kwa mwaka ulioishia Februari 2023 ilikuwa inauzwa kwa Sh114,762 kutoka Sh62,326 ya kipindi kama hicho mwaka 2022. 

Hilo ni sawa na ongezeko la Sh52,436 au na asilimia 84.1.

Ni kawaida katika kama hiki ambacho wakulima wanaendelea kuotesha mazao shambani, bei kupanda kwa sababu bidhaa za vyakula zinakuwa hazipatikani kwa wingi sokoni.

Kupanda kwa bei ya bidhaa hiyo kunawaumiza walaji kwa sababu wanalazimika kutoboa zaidi mifuko yao zaidi ili kupata zao hilo la chakula, wakati wakulima wananeemeka na bei hiyo.

Hata wakati bei ya mahindi ikipaa kwa asilimia 84.1 zaidi ya ile ya mwaka 2021, bei hiyo imekuwa ikipanda na kushuka tangu Machi mwaka jana. Mathalan, Januari mwaka huu bei ya mahindi ilikuwa Sh115,852 na mwezi uliofuata imeshuka hadi Sh114,762.  

Siyo tu mahindi, karibu bei za mazao yote ya chakula zimepanda ndani ya mwaka mmoja uliopita. 

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
25 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
25 May, 2026
No active movers today
Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

Nukta TV

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

Nukta TV

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

Nukta TV