Maeneo ya umma yapimwe kuepusha migogoro ya ardhi

May 12, 2023 12:39 pm · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Hiyo pia itasaidia maeneo hayo kutambulika kisheria.

Dar es Salaam. Kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi  (CCM) wilayani Misungwi, imeagiza ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo  kuhakikisha inapima maeneo ya taasisi za umma ili kuondoa migogoro ya ardhi inayoweza kujitokeza.

Akizungumza wakati alipofanya ziara ya kukagua na kutembelea miradi ya maendeleo kwenye wilaya hiyo, Mwenyekiti wa CCM wilayani humo, Michael Smart amemwagiza Mkurugenzi kuhakikisha anafanyia kazi suala hilo ili maeneo ya umma yaweze kutambulika.

Kauli ya Mwenyekiti hiyo imekuja baada ya taasisi za elimu ya sekondari Jitihada,  Misungwi na Kituo cha afya Koromije kueleza maeneo hayo kutotambulika mipaka halisi ya taasisi hizo hali inayosababisha wananchi kuyavamia.

Mkuu wa shule ya sekondari Jitihada, Rachel Matinde amesema miongoni mwa changamoto zinazoikumba shule hiyo ni pamoja na eneo la shule hiyo kutopimwa.

Changamoto hiyo pia ilielezwa na Mkuu wa shule ya sekondari Misungwi, Thomas Makoye ambaye alisema eneo hilo halijapimwa na halina uzio wa shule hali inayochangia wanafunzi wanaoishi bweni kukaa kwa wasiwasi.

” Tunaomba maeneo yetu yapimwe na tupatiwe hati ili tuyatambue kwakuwa kuna baadhi ya watu wanayavamia na kudai mipaka yao ndiko inakoishia,” amesema Rachel

Akizungumzia suala hilo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Kashinje Machibya amesema watalifanyia kazi suala hilo ili maeneo yote ya taasisi yapimwe.

Machibya amekiri kuwa maeneo mengi ya taasisi za umma hayajapimwa na mkakati ni kuhakikisha yaanza kupimwa na kupatiwa hati za umiliki.

” Kwa kuanza tunaanza kushirikisha kamati ya mipango miji ili ianze mchakato wa kupima maeneo yote ya taasisi za umma, vitendea kazi vya upimaji vipo ni suala tu la kuweka mipango vizuri,” amesema Machibya.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
21 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
21 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
21 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Nukta TV

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Nukta TV

FAHAMU KUHUSU SIKOSELI | Part 1: Ugonjwa wa kurithi, unaotesa maelfu ya watoto Tanzania

FAHAMU KUHUSU SIKOSELI | Part 1: Ugonjwa wa kurithi, unaotesa maelfu ya watoto Tanzania

Nukta TV