Sio kweli: Thabo Mbeki hajafariki dunia
Dar es Salaam. Kumekuwa na taarifa inayosambaa katika mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari Tanzania kuwa, Rais mstaafu wa awamu ya pili wa Afrika Kusini Thabo Mbeki amefariki dunia lakini habari hiyo haina ukweli wowote.
Taarifa za kifo cha Mbeki zilianza kusambaa leo Januari 3, 2024 katika mitandao tofauti tofauti ikiwemo mtandao wa kijamii wa X sambamba na baadhi ya magazeti na radio za hapa Tanzania pamoja vyombo vya habari vikubwa vya nje ya nchi
Ukweli ni huu
Nukta Fakti kupitia vyanzo mbalimbali vya habari vya ndani ya Afrika kusini na vingine vya kimataifa imethibtisha kuwa habari hiyo haina ukweli wowote.
Pia wakfu wa Thabo Mbeki (Thabo Mbeki Foundation) umetoa tarifa kupitia mtandao wa kijamii wa X (TMF foundation) ukieleza hali ya Afya ya Rais huyo mstaafu.
Ukiwa na kichwa cha habari Statement Regarding President Thabo Mbeki’s Health katika tafsiri isiyo rasmi (Taarifa ya afya kuhusu Rais Thabo Mbeki)
Katika taarifa hiyo kwa vyombo vya habari wamekanusha taarifa zinazosema Rais mstaafu Thabo Mbeki amefariki dunia kwa kuwa ni mzima wa afya.
Kwa hapa Tanzania gazeti la mwananchi lilikanusha habari hiyo kuwa haina ukweli wowote na kuomba radhi wasomaji wake kupitia chapisho kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram.