Upungufu wa umeme, unavyosababisha upotevu wa mapato, ajira viwandani Mwanza

December 7, 2023 2:08 pm · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Mameneja wa viwanda wabainisha kupoteza mamilioni ya fedha kutokana na kukatika kwa umeme mara kwa mara.
  • Mamia wapoteza ajira kutokana na ongezeko la gharama za uendeshaji.

Mwanza. Mameneja wa Viwanda jijini Mwanza wameiomba Serikali kushughulikia changamoto ya upungufu wa umeme, jambo linalochochea kukwama kwa shughuli mbalimbali za uzalishaji na kusababisha upotevu wa mapato na ajira.

Godfrey Samwel, meneja wa kiwanda cha kuchakata samaki cha Tanzania fish processors amemwambia Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Amos Makalla kuwa, pamoja na changamoto nyingine kukatika kwa umeme kumesababisha kushuka kwa shughuli za uzalishaji kutoka tani 120 mwaka 2011 mpaka wastani wa tani 12 hadi 15 kwa sasa.

Samwel amebainisha kuwa sambamba na upungufu wa samaki, gharama za kununua mafuta ya kuendeshea mitambo pale umeme unapokatika ni chanzo cha kushuka kwa uzalishaji.

Changamoto kama hiyo pia imeibuliwa na Meneja wa Kiwanda cha nguo cha Mwatex Mariam Msangi ambaye amebainisha kuwa  kukatika kwa umeme mara kwa mara kumesababisha harasa ya zaidi ya Sh100 milioni kwa mwaka.


Soma zaidi : Umemejua unavyookoa maisha ya wajawazito Iringa


Ajira zapungua viwandani

Kutokana na kuongezeka kwa gharama za uzalishaji kulikochangiwa na kutokuwepo kwa huduma ya uhakika ya umeme kwa siku za hivi karibuni ajira latika viwanda vingi zimepungua kasi na kuacha mamia ya watu bila ajira.

Mathalan, kwa mujibu wa Meneja wa kiwanda cha nguo cha mwatex Maruiam Sarungi, ajira zimepungua kutoka 800 na kufikia 500.

Aidha, katika kipindi cha miaka 10 iliyopita kiwanda samaki cha TFP kilikuwa kimeajiri wafanyakazi 500 lakini hadi sasa wamesalia wafanyakazi 300 pekee. Ambapo kati ya yao asilimia 40 ni wanawake.

Wakazi Mwanza wanena

Wakizungumza na Nukta habari,  wakazi jijini Mwanza ambao baadhi yao wamewahi kufanya kazi katika kiwanda hicho wamesema uchumi wao umeshuka ambapo kwa siku walikuwa wanalipwa kati ya sh7, 000 hadi 10, 000 na sasa hawapati kitu chochote.

“Lucia Amos mkazi wa mtaa wa Igogo  aliyekuwa akifanya kazi katika kiwanda cha TFP amebainisha kuwa awali alikuwa anaendesha maisha kwa ujira wa Sh7, 000 kwa siku  ambapo alimudu kuhudumia familia yake na sasa analazimika kufanya vibarua ambavyo si vya uhakika jambo lililoongeza ugumu wa maisha.


Soma zaidi : Ugonjwa wa kipindupindu waripotiwa Kagera, wanne wafariki


Kauli ya serikali

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Amos Makalla ameuagiza uongozi wa  Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) mkoani humo kuwa na ratiba inayofahamika ya mgao wa huduma zao ili wenye viwanda waweze kujipanga kwenye uzalishaji jambo litakalosaidia kupunguza hasara.

Itakumbukwa kuwa Septemba 23, 2023 Tanesco walitangaza uwepo wa changamoto ya upungufu wa umeme uliotokana na kupungua kwa maji katika vituo vya kuzalishia umeme pamoja na ongezeko la mahitaji ya nishati hiyo muhimu kwa ukuaji wa uchumi.

Hatua ya matumaini inayosubiriwa ni kuanza kutumika kwa bwawa la Mwalimu Nyerere litalokuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 2,115 za umeme ambapo Disemba 1, 2023 Tanesco wlaitangaza kuwa wanatarajia kuanza majaribio ya kuingiza umeme utaozalishwa na bwawa hilo kwenye gridi ya Taifa.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Nukta TV

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

Nukta TV

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Nukta TV