Mtindo huu wa maisha unaiweka afya yako hatarini

November 11, 2021 11:14 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni matumizi ya pombe, uvutaji wa sigara, matumizi ya vyakula vyenye mafuta na kutokufanya mazoezi.
  • Husababisha magonjwa ya kisukari, moyo, saratani, figo na shinikizo la damu. 

Dar es Salaam. Watanzania ambao wanaendekeza mfumo wa maisha usiofaa ukiwemo unywaji pombe uliopitiliza wametakiwa kuachana na tabia hizo kwa sababu wanachangia kuongezeka kwa magonjwa yasiyoambukiza na hivyo kupunguza nguvukazi ya Taifa.

Mkurugenzi Msaidizi wa Magonjwa yasiyoambukiza  Dk James Kiholongwe akizungumza wakati akitoa elimu kwenye wiki ya kudhibiti magonjwa yasiyokuwa yakuambukiza jijini Dodoma  amesema kuwa kuna kila sababu ya jamii kujizuia kuishi maisha yanayoweza kuathiri afya.

Dkt. Kiholongwe amesema kuwa, watu wengi ambao wamekithiri katika matumizi ya pombe, uvutaji wa sigara, matumizi ya vyakula vyenye mafuta na kutokufanya mazoezi wamejikuta kwenye wimbi la kupata magonjwa yasiyokuwa ya kuambukiza na kulibebesha Taifa mzigo mzito.

Ameyataja baadhi ya magonjwa hayo kuwa ni kisukari, ugonjwa wa moyo, saratani, figo na shinikizo la damu ambayo vichocheo vikubwa ni kuishi mtindo usiofaa wa maisha usioendana na ulaji wa vyakula na vinywaji vinavyotakiwa.

Aidha, Dk Kiholongwe ameitaka jamii kujenga utaratibu wa kufanya mazoezi na kupima afya mara kwa mara Ili kujua mwenendo wa afya kwani itasaidia kujiepusha na magonjwa hayo.

                         

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW