Tanzania, Misri zafungua ukurasa mpya wa kibiashara

April 28, 2022 8:19 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Emmanuel Tutuba (kushoto) akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mazungumzo na ujumbe wa Misri ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje w Misri, Dk Ranai Al-Mashat (kulia), Makao makuu ya Benki ya Dunia, Jijini Washington DC, Marekani. Picha| Wizara ya Fedha na Mipango.


  • Zajadiliana kuondoa vikwazo vya kikodi.
  • Wafanyabiashara kuongeza kasi ya kuuza bidhaa.

Dar es Salaam. Huenda kasi ya ufanyaji kati ya Tanzania na Misri ikaongezeka hivi karibuni na kuwanufaisha zaidi wananchi hizo mbili baada ya kuwepo kwa majadiliano ya kuondoa vikwazo vya kikodi.

Tanzania na Misri ziko katika hatua ya mwisho ya majadiliano ya kuipatia ufumbuzi changamoto ya utozaji kodi mara mbili kwenye bidhaa zinazoingia au kutoka katika nchi hizo mbili ili kusisimua biashara na kukuza mauzo nje ya nchi yatakayoongeza upatikanaji wa fedha za kigeni.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Emmanuel Tutuba ametoa kauli hiyo jana April 27, 2022 baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri, Dk Rania Al-Mashat, kando ya mikutano ya kipupwe ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Jijini Washington DC, Marekani.

Tutuba amesema kuwa majadiliano ya wataalam wa masuala ya kodi kutoka pande zote mbili yanaendelea na kuahidi kuwa ndani ya kipindi cha miezi miwili yatakuwa yamekamilika na kuwashauri viongozi wa juu wa nchi kuhusu hatua zilizofikiwa ili kuondoa changamoto hiyo kwa lengo la kuboresha biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Misri.

Kuhusu uwekezaji na ukuzaji biashara, Tutuba amehakikishia Dk  Al-Mashat, kuwa Serikali imeweka mazingira mazuri ya uwekezaji na kutoa wito kwa kampuni na mashirika ya Misri kuja kuwekeza Tanzania.

Ziara iliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan nchini Misri hivi karibuni iliwezesha kupatikana kwa wawekezaji 120 ikiwemo kampuni ya kuzalisha vifaa vya umeme zikiwemo transfoma, ya Elsewedy Electric East Africa.

Katika hatua nyingine, Tanzania imeahidi kuiunga mkono Misri kuandaa Mkutano wa 27 wa Mabadiliko ya Tabianchi unaotarajiwa kufanyika nchini humo wenye lengo la kutafuta fedha, teknolojia na uwezeshaji kwa ajili ya kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi hususan katika nchi za Afrika.

Kwa mujibu wa Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, biashara baina ya nchi hizo mbili imeongezeka kutoka Sh84.3 bilioni mwaka 2018 hadi kufikia Sh87.3 bilioni mwaka 2020 hivyo kuna kila sababu yakuendeleza majadiliano na makongamano ya biashara baina ya nchi hizo mbili ili kutoa fursa kwa wafanyabiashara kutumia fursa za uwekezaji.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri, Dk Al-Mashat amesema kuwa Misri ni mdau mkubwa wa maendeleo wa Tanzania na itaendelea kutoa ushirikiano.

Nchi ya Misri imekuwa ikitekeleza miradi mbalimbali ya kimkakati katika nchi ya Tanzania ukiwemo ujenzi wa mradi wa Bwawa la Kufua Umeme wa Maji la Julius Nyerere (JNHPP-MW2115) unaotarajiwa kukamilika mwezi Juni 2022 na kusaidia viwanda kuzalisha kwa uhakika.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
31 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
31 May, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

Nukta TV

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

Nukta TV

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

Nukta TV