Bilionea Elon Musk auza sehemu ya hisa za Tesla

August 11, 2022 1:56 pm · Davis Matambo
Share
Tweet
Copy Link
  • Amelenga kuepuka mauzo ya dharura ya hisa hizo kwa sababu ya kutokuwa na uhakika juu ya kesi ya ununuzi wa Twitter.

Huku akiwa katika mzozo wa kisheria wa ununuzi wa mtandao wa  Twitter, tajiri namba moja duniani Elon Musk ameamua kuuza sehemu ya hisa zake katika kampuni yake ya Tesla ili kijihakikishia kiasi cha pesa kitakachomuweza kukamilisha dili hilo.

Agosti 10 mwaka huu gazeti la The Wall Street Journal (WSJ) lilipoti kuwa Elon Musk ameuza hisa za Tesla zenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 6 sawa na Sh16.1 trilioni ili kuepuka mauzo ya dharura ya hisa hizo endapo atalazimika kuinunua Twitter.

Uuzaji wa hisa za kampuni hiyo ya magari ya umeme unakuja huku kukiwa na sintofahamu juu ya hatma ya mpango wa Musk kuinunua Twitter kwa Dola za Marekani bilioni 44 sawa na Sh102.6 trilioni.

Kupitia twitter Musk amesema amelenga kuzuia uuzaji wa dharura wa hisa ikiwa atalazimika kukamilisha mchakato wa ununuzi wa mtandao huo wa kijamii ambao alishitisha mwezi uliopita.

Mzozo kati ya Musk na Twitter ulianza mwezi Aprili, wakati ilipowekwa wazi kuwa ununuzi wa hisa za mtandao huo wa kijamii utampa Musk umiliki kwa asilimia 9.2 ya kampuni hiyo.

Miezi miwili baadaye Musk alitaka kujiondoa kwenye mpango wa ununuzi wa Twitter akilalamikia uwepo wa akaunti feki ambao alisema unaweza kuleta changamoto ya kimapato hapo baadaye.

Bilionea huyo anakabiliwa na kesi katika Mahakama ya Chancery ya Delaware nchini Marekani baada ya uongozi wa Twitter kumshitaki ili kumlazimisha kuinunua kwa sababu tayari mchakato wa ununuzi ulikuwa umeanza.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
26 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
26 May, 2026
No active movers today
Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

Nukta TV

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

Nukta TV

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

Nukta TV