Mkemia Mkuu kuongeza kibano wasambazaji haramu wa zebaki Tanzania

August 23, 2022 11:42 am · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Ndani ya mwaka mmoja zaidi ya tani 500,000 za zebaki zimeingizwa nchini kati ya Septemba 2021 na Agosti 2022 kupitia wasambazaji halali.
  • Mamlaka zabaini kuwa bado kuna wasambazaji wengine haramu sokoni.
  • Zebaki ni miongoni mwa kemikali hatari zinazotumika zaidi viwandani na majumbani Tanzania ikiwemo migodi ya wachimbaji wadogo wadogo. 

Mwanza. Katika kudhibiti matumizi holela ya zebaki nchini, Mmlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) imezitaka kampuni pamoja na watumiaji wa kemikali hiyo kujisajili kabla ya kujitosa kuziuza na kuzinunua sokoni.

Zebaki ni miongoni mwa kemikali hatari zinazotumika zaidi viwandani na majumbani Tanzania hususan katika uchenjuaji wa dhahabu katika migodi ya wachimbaji wadogo wadogo.

Mkemia Mkuu wa Serikali Fidelice Mafumiko amesema wapo baadhi ya wafanyabiashara wanaouza bidhaa hizo kinyemela licha ya kuwa ni hatari kwa afya za binadamu pale zinapotumika kinyume na taratibu.

“Ninaelekeza wadau wote wanaojihusisha na zebaki ikiwemo watumiaji ambao hawajasajiliwa…wafuate taratibu za sheria na kanuni katika ununuzi, uuzaji, utumiaji na usambazaji wa kemikali hiyo ili kuwalinda watumiaji wa sasa na vizazi vijavyo,” amesema Dk Mafumiko katika mkutano na wadau wa kemikali uliofanyika jijini Mwanza Agosti 22.

Usajili wa wasambazaji wa zebaki umesaidia kubaini uingizaji wa kemikali hiyo na kutoa fursa kwa mamlaka kudhibiti matumizi holela.

Katika kipindi cha mwaka mmoja kati ya Septemba 2021 hadi Agosti 2022 zaidi ya tani 500,000 za zebaki zimeingiwa nchini kihalali na wasambazaji waliotambuliwa kwa mujibu wa Dk Mafumiko.

Amesema zebaki ni miongoni mwa kemikali zinazohatarisha zaidi afya za watumiaji duniani kutokana na kudumu katika mazingira kwa muda mrefu na kusafiri katika masafa marefu ya njia ya hewa maji na udongo hivyo kuathiri afya ya binadamu na mazingira.

Mkemia Mkuu wa Serikali, Dk Fidelice Mafumiko akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa maelekezo kwa wauzaji haramu wa zebaki nchini Tanzania kuacha mara moja na kufuata taratibu za usajili. Picha|Mariam John/Nukta.

Kemikali hiyo, ameeleza ina athari katika mfumo wa ufahamu, viungo vya binadamu kama figo, ini pamoja na mfumo wa uzazi hasa zaidi kwa akina mama wajawazito na watoto.

Katika kudhibiti kiwango cha matumizi ya kemikali katika migodi midogo midogo, amesema Serikali imeshaanza kuchukua hatua za kuhamasisha matumizi ya teknolojia mbadala wa zebaki katika uchenjuaji wa dhahabu ikiwemo kutumia kemikali mbadala aina ya Sodium Cyanide na kuchoma moja kwa moja udongo wenye dhahabu (Direct smelting).

Mara nyingi wafanyabiashara wanaoingiza kinyemela kemikali huwa hawafuati taratibu za kiusalama jambo ni hatari kwa afya zao na watu wanaozinunua.


Zinazohusiana: 


Mkemia wa kampuni ya Machugu Investment iliyopo mkoani Mwanza, Kenedy Kisinja ameipongeza Serikali kwa kuongeza ushirikiano na wadau wanaojihusisha na biashara ya kemikali ikiwemo zebaki.

Kudhibiti athari kwa watu na mazingira, Kisinja ameshauri Serikali kusimamia ipasavyo utaratibu wa kuhakikisha kampuni zote au taasisi zinazohusiana na uuzaji wa kemikali zinaajiri watalamu wenye sifa za kutumia Kemikali.

“Tunaiomba ofisi ya mkemia mkuu wa Serikali iendelee na mikakati mbalimbali ya utoaji elimu kuhusiana na matumizi ya zeba

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Nukta TV

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

Nukta TV

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Nukta TV